Usiwe Mchoyo, Wajulishe Rafiki Zako Kuhusu Betika

GAZETI lako la kijanja Betika lipo mikononi mwako kwa mara ya nne sasa. Tunajivunia wewe kuwa msomaji wetu ambaye unafaidika kupitia maujanja yaliyomo ndani yake.

 

Wewe ni wa thamani sana, uamuzi wako wa kuwa msomaji wetu kwa hakika ni sahihi kabisa na hautaujutia.

Jambo moja la msingi, sisi Betika tunaomba kutoka kwako; shea na rafiki zako kuhusu gazeti hili kwamba linapatikana kila Jumatano bure.

 

Wajulishe kuwa lipo gazeti la wajanja ambalo linatoa mwongozo sahihi wa mechi zote za wikiendi ambazo ni msaada kabla ya kufikiria kutandaza mkeka wako.

Ni imani yetu kwamba namba za kampuni mbalimbali zilizopo kwenye gazeti hili, odds na misimamo vina faida kwako.

 

Aidha, tunaendelea kuwakaribisha watangazaji wa kampuni mbalimbali za kubeti na lotto kutangaza nasi kwani kuna mafanikio makubwa.

 

Hata watangazaji wengine nje ya betting na lotto, milango ipo wazi kwenu kwani tunaamini, mtu akishinda kitita chake atahitaji kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali.

 

Sambaza taarifa hizi kwa watu wengi kadiri utakavyoweza. Kwa watangazaji wapya, tafadhali wasiliana na idara yetu ya masoko na matangazo kwa namba zilizopo kwenye Bodi ya Uhariri ya gazeti hili.

Endelea kuburudika na Betika.

Toa comment