USIYIYAJUA TUZO ZA SZIFF MSIMU WA PILI

BAADA ya kufanyika kwa kishindo msimu wa kwanza mwaka jana mbele ya mgeni rasmi, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, msimu huu wa 2019 Tuzo za Sinema Zetu nchini zijulikanazo kama Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) zimezinduliwa rasmi Septemba mwaka jana na zinatarajiwa kufanyika Februari 23, mwaka huu.  

GLOBAL MOVIES: CHANZO NI WEWE (PART ONE)

 

Katika tuzo hizi ndani ya msimu huu kuna mambo mengi ambayo huyajui lakini Showbiz Xtra limekuandalia.

  1. Mlezi Jokate

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ametangazwa kuwa mlezi wa Tuzo za SZIFF kwa msimu wa pili na kuahidi kuhamasisha vijana kujikita zaidi katika ubunifu wa sanaa ya uigizaji.

 

  1. Vigezo vyaanikwa

Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media ambao ndiyo waandaaji wa tuzo hizo, Tido Mhando alisema filamu zitashindanishwa kwenye vipengele tofauti huku ushindani ukiaminika kuwa mkubwa zaidi wa msimu uliopita kwa kuwa moja ya vigezo vya filamu zitakazoshindanishwa ni kuwa lazima ziwe zimeandaliwa kati ya mwaka 2016 hadi 2018.

  1. Vipengele kuongezwa

Tido alisema kuwa, mbali na hilo kwa mwaka huu wameo-ngeza vipengele vingine vitano na kufikisha idadi ya tuzo zinazowaniwa kuwa 24, pamoja na mshindi kuondoka na tuzo hiyo pia atakabidhiwa kiasi cha fedha taslimu kulingana na nafasi alizowania na kushinda.

 

GLOBAL MOVIES: CHANZO NI WEWE (PART TWO)

 

  1. Global TV yaweka rekodi

Kwa mara ya kwanza mara baada ya kuzinduliwa, Global TV Online ambayo ni televisheni namba moja mtandaoni imeweka rekodi ya kuingiza wasanii katika tuzo hizo. Ikum-bukwe kuwa, Global TV imekuwa ikirusha filamu za Kibongo na miongoni mwao ambazo ni Coretha, Chanzo Ni Wewe na Ardhi ya Damu zime-ingia moja kwa moja kwenye tuzo hizo sambamba na wasanii wake.

 

  1. Global TV yatoa wakali 5

Kama ulikuwa hujui, katika tuzo hizo Global TV imetoa waigizaji watano yaani wanawake wawili katika kipengele cha Msanii Bora wa Kike, Magreth Francis, Rhoida Richard na upande wa wanaume katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume ni Emmanuel Maasa, Surej Yusuph na Sango Johannes.

 

  1. Kupiga kura rahiiiisiii

Kura yako ni muhimu na ni rahisi kwani dirisha linatarajiwa kufungwa mwishoni mwa mwezi huu wa Januari hivyo unaweza kuwapigia wakali wa Global TV Online kwa kuingia katika simu yake upande wa kuandikia meseji. Msanii Bora wa Kiume, andika BM kisha acha nafasi andika 1000, acha nafasi kisha andika *8 na utume kwenda namba 0683 520006 utakuwa umempigia kura Emmanuel Maasa aliyecheza Filamu ya Coretha. Msanii Bora wa Kike, Rhoida andika BF acha nafasi kisha andika 760, acha nafasi andika *9 kisha tuma kwenda namba 0683 520006.

GLOBAL MOVIES: CORETHA (PART ONE)

 

Kupigia kura Filamu Bora ya Mwaka kupitia Filamu ya Ardhi ya Damu andika 760 kisha acha nafasi, andika *9 na tuma kwenda 0683 520006. Filamu ya Chanzo Ni Wewe andika 360 kisha cha nafasi, andika *7 na utume kwenda 0683 520006. Filamu ya Coretha andika 1000 kisha acha nafasi, andika *8 na utume kwenda 0683 520006.

 

GLOBAL MOVIES: CORETHA (PART TWO)

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO


Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment