Usiyoyajua Mtoto wa Mondi na Tanasha!

HATIMAYE Oktoba 2, 2019, mwanamama mtangazaji na mwanamuziki Tanasha Donna Oketch, raia wa Kenya alijaliwa mtoto mwanamume.

Tanasha ni mchumba wa mwanamuziki wa kimataifa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Ndiye aliyezaa naye mtoto huyo ambaye hadi sasa haijajulikana jina lake.

Ni rasmi sasa familia ya Diamond au Mondi imeongezeka. Kutoka idadi ya watoto wanne na sasa ana watoto watano. Kati yao mmoja tu ni wa kike, Tiffah Dangote.

 

Yupo mmoja anayesemekana yupo jijini Mwanza aliyezaliwa wakati Mondi hajawa staa mkubwa. Wengine wawili amezaa na mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tiffah Dangote na Prince Nillan. Mmoja na mwanamitindo Hamisa Mobeto, Dyllan na wa mwisho ni huyu wa Tanasha.

 

Kabla ya kuzaliwa mtoto wa Tanasha kulipita stori nyingi. Mtandao mmoja ulidai Tanasha alikuwa amejifungua mtoto akawa ni bahati mbaya, lakini baadaye mwanamama huyo alikanusha na kudai kuwa aliyemzushia mwanaye kifo alifanya jambo baya mno!

Yafuatayo ni usiyoyajua kuhusu mtoto huyo wa Mondi na Tanasha;

 

MTOTO WA KIUME

Ilifahamika mapema tu kuwa ujauzito aliobeba Tanasha ulikuwa ni wa mtoto wa kiume. Tanasha aliliweka wazi mapema tu baada ya kupiga picha na nguo za rangi ya bluu-bahari kisha kufuatiwa na baby shower ambayo nayo mavazi yake yake watu walitupia rangi ya bluu-bahari. Kwa tunaoelewa hayo mambo tulijua ni mtoto wa kiume!

 

SAA 17 LEBA

Kwa waliopita leba wanasema kukaa ndani yake kwa sasa moja tu ni maumivu tosha. Lakini Tanasha yeye alikaa kwa sasa 17 na kujifungua kwa njia ya kawaida! Wataalam wa mambo hayo wanasema Tanasha ni mwanamke imara mno.

 

AZALIWA SIKU MOJA NA BABA’KE

Ni jambo la nadra sana. Watu wawili kwenye familia moja kugongana siku au tarehe ya kuzaliwa. Wote, Mondi na mwanaye sasa watakuwa wanafanya sherehe ya kuzaliwa pamoja kwani wote wamezaliwa Oktoba 2.

 

Kuna madai yalienea kuwa Tanasha alijifungua siku nyingi kabla ya siku hiyo, lakini alisubiri kutangaza ili kutengeneza jambo hilo.

Hata hivyo, Tanasha alikanusha vikali taarifa hizo kwa kutoa kadi na dokyumenti za Hospitali ya Aga Khan jijini Dar, zikionesha alijifungua siku hiyo.

 

BABA’KE ATIMIZA MIAKA 30

Mondi sasa ni baba wa watoto watano kama alivyo Zari ambaye ni mama wa watoto watano. Kama baba, Mondi sasa ana umri wa 30. Ni wakati sasa wa kutulia na kuwaweka pamoja wanaye ambao wamesambaa wakilelewa na mama zao (single mother), jambo ambalo halina afya kwa malezi ya wanaye.

 

WATANO KWA MONDI, WA KWANZA KWA TANASHA

Kama ulikuwa hujui, mtoto wa Tanasha ni wa tano kwa Mondi na wa kwanza kwa Tanasha mwenye umri wa miaka 24. Kuna mambo ya usichana ambayo sasa Tanasha atapaswa kuyaacha kwa maana ya kuwa mama.

 

ISHU YA JINA

Mapema tu, Mondi na Tanasha walisema jina la mtoto wao litakuwa ni sapraiz. Mtoto huyo hawezi kuendelea kuitwa mtoto wa Tanasha hivyo matarajio ya wengi ni kutangazwa kwa jina ambalo wengi wanaamini litakuwa la kipekee na kwamba mara tu baada ya kutangazwa mtoto huyo atakuwa bonge la staa pale jina hilo litakapotamkwa. Yetu ni macho na masikio!

 

URAIA WA MTOTO

Tofauti na utata ulioibuka kwa watoto wengine wa Mondi aliozaa na Zari, Tiffah na Nillan ambao ni raia wa Afrika Kusini, huyu wa Tanasha ni raia rasmi wa Tanzania pamoja na kwamba mama yake ni raia wa Kenya. Ukweli ni kwamba baba ni Mtanzania na Tanasha amejifungulia Tanzania.

 

NYUMBA 2

Hata kabla ya kuzaliwa, wakati wa baby shower ya Tanasha, Mondi alitangaza kwamba mara tu baada ya kuzaliwa atamnunulia nyumba za kifahari mbili kwenye majiji makubwa Afrika Mashariki; Nairobi, Kenya na Dar es Salaam, Tanzania.

 

MTOTO STAA KULIKO WOTE

Mtoto huyo wa Mondi na Tanasha anatajwa kuwa ndiye atakayekuwa mtoto staa zaidi kutokana na mipango ya wazazi wake ya kumpaisha kwa lengo la kuwazima wale wa Zari, Tiffah na Nillan ambapo kwa sasa Tiffah ndiye anatajwa kuwa staa zaidi Afrika Mashariki.

Makala: Sifael Paul


Loading...

Toa comment