The House of Favourite Newspapers

Usome Hapa Waraka wa Edward Lowassa kwa IGP Mangu

0

Lowassa
Mhe. Edward Ngoyai Lowassa.

Kwako Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP)

Salaam,

Kwanza niwie radhi kwamba nimelazimika kwa nafasi yako na yangu, kukiuka taratibu za kiitifaki hata nikalazimika kuandika waraka huu kwako.

Ninafanya hivyo si kwa sababu yoyote, bali kwa sababu tu jambo au mambo yaliyonisukuma kukukifikishia ujumbe huu, yana uzito mkubwana kimsingi yanaweza kuathiri mustakabali mwema wa kitaifa.

Msingi wa waraka wangu huu ni agizo ulilotoa wewe, Inspekta Jeneraliwa Polisi la kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa namaandamano ya vyama vya upinzani.

Ni bahati mbaya kwamba wakati ukitoa maagizo hayo, nilikuwa niko njeya nchi, ingawa kwa bahati njema, Watanzania wenye mapenzi mema nataifa lao waliopo hapa nchini na nje, walinifikishia taarifa juu ya agizolako hilo.

IGP, siyo desturi yangu kuandika waraka wa namna hii mtandaoni au kupitia vyombo vya habari, ingawa safari hii nimelazimika kufanyahivyo ili kuweka rekodi sahihi, sambamba na kukosoa sababu ulizotoakuwa nyuma ya agizo lako hilo.

Wakati nikiwa natafakari kwa mshangao agizo lako hilo, na baadayekurejea nyumbani, nilipigwa na butwaa zaidi niliposikia Jeshi la Polisi tena katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, likiwazuia viongozi wetu wakuuna wa juu kitaifa kufanya mikutano ya hadhara.

Agizo hilo lilifuatiwa na tukio la kukamatwa, kushikiliwa na kuhojiwakwa viongozi hao, akiwamo mwenyekiti wetu wa taifa, Freeman Mbowe(MB) huko Mwanza hivi majuzi.

Katika matukio hayo yote, Polisi mnadai kuwa na taarifa zakiintelijensia ambazo zinazonyesha kuwapo kwa uwezekano wa kutokeakwa vurugu kwenye mikutano hiyo ya hadhara ya vyama vya siasa.

Madai haya ya polisi ambayo hata wewe binafsi umepata kuyatoa awaliulipoamua kwa sababu mnazojua ninyi wenyewe, kuminya haki zamsingi na za kikatiba za vyama vya siasa kujumuika na kutimizamajukumu yao ya kisiasa hayana ukweli hata kidogo.

Si hivyo tu, uzoefu wa kihistoria unakinzana na kwenda kinyume kabisana madai hayo, kwani yako matukio mengi ambayo yamethibitishakwamba mijumuiko ya wanasiasa wa vyama vya upinzani, yakiwamomaandamano na hata mikutano imekuwa ikifanyika kwa amani.

Iko mifano mingi inayoonyesha kwamba, tumefanya shughulimbalimbali za kisiasa kwa maana ya maandamano na mikutano yahadhara kwa amani na pasipo kuwapo hata kwa ulinzi wa polisi.

Mifano ya namna hiyo ndiyo inayosababisha baadhi yetu si tu tupinganena maagizo yanayotoa mwelekeo wa kukandamizwa kwa uhuru wakikatiba wa vyama vya siasa vya upinzani kujumuika bali kwenda mbalizaidi na kutilia shaka hata maagizo hayo na kuyaona kuwa na misukumoiliyojificha nyuma ya kichaka cha ‘sababu za kiintelejensia’.

Naandika waraka huu kwako nikiamini kwa dhati kabisa kwamba, kilekilichotokea Kenya hivi karibuni ambako mahakama ilitupilia mbalimaagizo ya namna hii ya polisi kujaribu kuzuia haki ya kikatiba yavyama vya upinzani kuandamana ndicho kinachoelekea kutokea hatahapa kwetu pia.

Si hilo tu, naamini wewe IGP ulifuatilia kile kilichotokea Uganda sikuchache tu baada ya Rais Yoweri Museveni kutangazwa mshindi wa urais ambako chama kimoja cha siasa kiliitisha mkutano wa hadhara nakikamwapicha Besigye ambaye wao wanaamini ndiye aliyeshinda urais.

Waganda hao ambao wamekuwa wakiiamini kwamba mgombeawanayemuunga mkono ndiye aliyeshinda japo kura zake ziliibwa, waliruhusiwa kuandamana na kukutana kwa uhuru ingawa baadayewalikamatwa.

Ni jambo la kujifunza kwamba, Waganda hawa hawakuzuiwa na‘kuwapo kwa taarifa za kiinteligensia’ licha ya kwamba walishtakiwabaadae.

Tunachojifunza hapa ni mamlaka za dola, kama lilivyo jeshi letu la polisi, kuheshimu na kulinda haki za raia na kuepuka hatari ya vyombovyetu kujipa dhamana ya kuwaamulia wananchi masuala yao kwakisingizio cha taarifa za kiintelijinsia.

Je, kwa maagizo ya namna hii, Inspekta Jenerali Mangu na wenzakopolisi mnatuonaje sisi viongozi wa upinzani?

Je, mnafikiri pamoja na uzoefu wetu katika siasa na uongozi tunawezatukawa mbumbumbu wa kutambua haki zetu au hata kushindwa kujuadhamana kubwa tuliyobeba ya kuwatumikia wananchi na taifa letu?

Je, IGP Mangu na wakuu wenzako wa Jeshi la Polisi mnapotoa maagizoya namna hiyo hamuoni kwamba mnajenga taswira tu kwamba, malengoyenu ni kutafuta jinsi ya kutumia magari ya upupu yaliyoagizwa kwapesa nyingi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana?

Je, mmeshindwa kujifunza kwamba, kama kulikuwa hakuna vurugukabla na baada ya Uchaguzi Mkuu pamoja na kuwapo kwa kila viashiriavilivyochochewa na taasisi za dola, wapinzani hatuna sababu hata mojaya kuwa chanzo cha vurugu za namna hiyo?

IGP Mangu, pengine ni busara nikakukumbusha kwamba, vyama hivihivi vya upinzani chini ya mwavuli wa UKAWA viliwahi kuandamanakwa maelfu kutoka Buguruni yaliko makao makuu ya CUF hadi makaomakuu ya CHADEMA Kinondoni kwa amani na kwa utulivu.

Je, hukumbuki kwamba katika maandamano hayo yaliyohusisha maelfuya wakazi wa Dar es Salaam, hakuna hata sindano ya wananchiiliyopotea wala mtu kukwaruzwa?

Hayo na mengine mengi ndiyo ambayo yamenifanya nitafakari sana nakukosa jibu naposikia polisi mkituzuia kwenda vijijini kuwashukuruwananchi kwa kutuheshimu na kutupiga kura zao

Ni nini hicho kitakachoathiri amani na utulivu? Wanachama wa vyamavipi hao ambao eti watapingana kwa sababu sisi tumeamuakuwashukuru wananchi waliotuunga mkono kwa mamilioni?
IGP Mangu, nakuomba uyatafakari haya na kuliangalia upya agizo lako, ambalo yumkini haliitakii mema nchi yetu.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika
Edward Ngoyai Lowassa

Leave A Reply