The House of Favourite Newspapers

Ustaa una raha yake wadogo, umaarufu mkubwa

0

north-west-ballet-bun

North West.

WAKATI watu mbalimbali wakihangaika kutafuta umaarufu kwa njia nyingi hadi wengine kufikia hatua ya kujidhalilisha kwa kujinadi nusu utupu, kwa baadhi ya watu hasa watoto wa mastaa ni tofauti sana kwa kile kinachotajwa kama kuzaliwa na bahati kubwa ya kuwa na umaarufu kupitia wazazi wao.

Blue Ivy.

Baadhi ya watoto hao kinyumbaninyumbani na mamtoni ni kama wafuatao:Blue Ivy Ni mtoto pekee wa mwanamuziki Beyonce na Jay-Z, umaarufu wake ulianza tangu ujauzito ambapo vyombo vingi vya habari viliripoti taarifa zake.

Kwa sasa akiwa na umri wa miaka mitatu, anatajwa kama mtoto maarufu zaidi duniani huku nyota yake kwenye mambo ya burudani hasa fasheni na muziki ikionekana kuwaka vilivyo. Amewahi kushiriki kwenye wimbo wa mama yake, Beyonce uitwao ‘Blue’ na kupanda mara kadhaa jukwaani akiimba na kucheza kwenye shoo za wazazi wake bila uoga.North West Huyu ni mtoto wa kike wa Rapa Kanye West na mwanamitindo, Kim Kardashian.

North anaingia katika listi hii kwa kiwango cha mitandao ya habari iliyoandika tangu wakati akiwa tumboni mwa mama yake. Lakini pia North ambaye sasa ana miaka miwili, ameonekana kuwa mwanamitindo kutokana na nguo kumkaa vizuri huku naye akipitia kiki ya kutokea kwenye video ya baba yake inayojulikana kwa jina la Only One.

Tiffah

Tiffah Kichanga huyu wa mkali wa Bongo Fleva,Diamond Platnumz na mwanamama tajiri,Zari, anatikisha Kibongobongo kuanzia historia yake kabla hajazaliwa na mpaka akiwa anatimiza siku 40. Kwa umri huo mdogo ameonekana kuwa maarufu zaidi baada ya kupata followers’ zaidi ya 126,000 kwenye mtandao wake wa Instagram, huku kila mtu akitamani kumuona sura yake ambayo ilikuwa ikifichwa kwa muda mrefu.

Mbali na hayo taarifa ni kuwa mtoto huyo amekula dili la kuwa Balozi wa Pugu Mall na Msasani City Mall kwa upande wa maduka ya nguo za watoto ambapo anavishwa bure kwa mwaka mzima jambo ambalo halijawahi kutokea kwa mtoto mwingine wa staa wa Bongo.

Royalty Tofauti na watoto wa mastaa wenzake, mtoto huyu wa mwaka mmoja wa staa, Chris Brown na mwanadada Nia Guzman,pengine hakupata sana nafasi ya kuwashinda watoto wengine kutokana na taarifa za uwepo wake kuibuka ghafla mapema mwaka huu, lakini hiyo haizuii kuingia kwenye listi hii kutokana na umaarufu wa Chris Brown anayeonekana naye mara kwa mara huku kesi ya kugombea haki ya kuishi naye ikikuza jina la mtoto huyo.

Royalty.

Kwa sasa Chris ameshinda kesi hiyo na amepata haki ya kuishi naye.Tanzanite Ni mtoto wa mwanamuziki, H-Baba na mcheza filamu, Flora Mvungi.Kwa sasa ana miaka mitatu na amekuwa mmoja wa watoto maarufu wa mastaa  ongo kupitia wazazi wake huku akipata ‘followers’ zaidi ya 14,000 kwenye mtandao wa Instagram huku wazazi wake hao wakimtengeneza muonekano wa masuala ya fasheni zaidi na muziki ambapo kwa sasa anafundishwa kupiga kinanda.

 

Leave A Reply