The House of Favourite Newspapers

UTAJIRI ALIOUACHA MUGABE USIPIMEE!

WAKATI Zimbwabwe na Afrika nzima ikiendelea kuomboleza msiba wa kiongozi wake shupavu, Rais wa pili wa nchi hiyo, Robert Gabriel Mugabe (95), Gazeti la Ijumaa Wikienda linakujuza mengi zaidi ya kiongozi huyo ikiwemo utajiri wake. Mugabe alifariki dunia Septemba 6, mwaka huu nchini Singapore barani Asia alipokuwa amelazwa akipigania uhai wake tangu Aprili, mwaka huu.

UTAJIRI WAKE

Kwa mujibu wa mtandao maarufu kwa habari za mastaa wa Afrika Kusini, Mugabe anatajwa kuwa na utajiri wa zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 1 (zaidi ya shilingi trilioni 2.3.)

Pamoja na mitandao mingi inayoaminika kumtaja kuwa na utajiri huo, ipo mitandao mingine inayomtaja Mugabe kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani milioni 20 (zaidi ya shilingi bilioni 45.6) Inaelezwa kuwa, utajiri wa Mugabe upo ndani ya Zimbabwe, lakini pia nje ya nchi hiyo amewekeza katika miradi mbalimbali.

MASHAMBA

Upande wa vyama vya upinzani nchini Zimbabwe, unamtaja Mugabe kuwa anamiliki mashamba makubwa 14 nchini humo likiwemo shamba maarufu kwa jina la Omega Diary Farm, shamba kubwa zaidi ukanda wa Kusini mwa Afrika.

MAJUMBA, MAGARI

Pia inaelezwa kwamba Mugabe ameacha majumba na magari ya kifahari. Zimbabwe pekee, inaelezwa anamiliki nyumba 6 za kifahari ikiwemo ile maarufu kwa jina la The Blue Roof inayokadiriwa kuwa na thamani ya Dola ZA Kimarekani milioni 10 (zaidi ya shilingi bilioni 2)

SIFA ZAKE SASA…

Mjengo huo matata wenye eneo la takriban ekari 44, una vyumba vya kulala visivyopungua 25, mabwawa mawili ya kuogelea na sebule kama ‘uwanja wa taifa’ yenye uwezo wa kukaliwa na takriban watu 30 kwa wakati mmoja.

MAGARI SASA…

Miongoni mwa magari ya kifahari anayodaiwa kumiliki Mugabe ni pamoja na Rolls Royce na Mercedes Benz S600L Pullman. Gari hilo limedizainiwa maalum ambapo lina uwezo wa kutembea lilometa 50 likiwa limepata pacha ya risasi na aliyeko ndani anaweza kuzungumza na watu walioko nje ya gari wakasikia bila ya yeye kufungua vioo.

Gari hilo lina kila aina ya ulinzi, ambapo licha ya kuwa na usiri mkubwa juu ya gharama alizotumia kutengenezewa gari hilo maalum, lakini linatajwa kuwa na thamani ya Dola za Kimarekani milioni 1.2. Mbali na magari mengine ya kifahari, Mugabe pia anatajwa kumiliki boti, samani za ndani za dhahabu na saa ya bei mbaya.

ZAIDI KUHUSU MUGABE

Mugabe alikuwa ni mtu wa dini, wazazi wake wote wa walikuwa Wakatoliki, hivyo alilelewa kwenye misingi ya Kikatoliki. Kwa mujibu ripoti ya CNN, Februari 2010, Mugabe alisherehekea bethidei yake iliyomgharimu takriban Dola za Kimarekani 300, 000.

NUKUU ZAKE MAARUFU

Marehemu Mugabe alikuwa maarufu zaidi kwa nukuu zake. Zipo ambazo alikuwa akizungumza yeye mwenyewe, lakini baadhi zilikuwa zikiandikwa na watu mbalimbali wanaomfuatilia mzee huyo.

Miongoni mwa nukuu zake maarufu ni pamoja na; ‘The only white man you can trust is a dead white man’ akiwa na maana mzungu pekee unayeweza kumuamini ni yule aliyekufa. Nyingine ilikuwa hii; ‘I have died many times. I have actually beaten Jesus Christ because he only died once.” (Nimezushiwa kifo mara nyingi kuliko hata Yesu ambaye alikufa mara moja tu).

Kuna hii; ‘We dont mind sactions banning us from Europe. We are not Europeans.’ (Hatujali kuwekewa vikwazo na nchi za Ulaya. Sisi si Wazungu).

HISTORIA YAKE

Mugabe alizaliwa Februari 21, 1924 katika Kitongoji cha Kutama, Kusini mwa Rhodesia (sasa Zimbabwe). Ni mtoto wa fundi uashi/seremala (Gabriel Matibiri) na alisomea ualimu katika shule za seminari. Baada ya kuhitimu, alijiingiza na kupata umaarufu wa kisiasa alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Fort Hare, Afrika Kusini.

Alihitimu Shahada ya Uchumi mwaka 1958, lakini alifanya kazi ya ualimu nchini Ghana hadi mwaka 1960. Pia alifundisha Chuo cha Mtakatifu Mary ambako alikutana na mke wake wa kwanza Sarah Heyfron. Walikuwa marafiki na baadaye mwaka 1961 wakafunga ndoa takatifu, lakini hata hivyo, mkewe huyo alifariki dunia mwaka 1992. Agosti 17, 1996, Mugabe alioa mke wa pili, Grace Marufu.

Mwaka 1960 ndiyo mwaka aliorejea nchini mwake na kusaidiana na Ndabaningi Sithole kuunda Chama cha Zimbabwe African Nation Union (ZANU), lakini umaarufu wake uliibuka alipojiunga na Chama cha National Democratic Party ambacho baadaye kilifahamika kama Zimbabwe African People (ZAPU).

Alikaa hapo kwa muda hadi pale alipoanzisha Zimbabwe African National Union (ZANU). Mugabe na chama chake aliingia kwenye machafuko na Chama cha ZANU ambayo yalimsababisha afungwe jela kwa miaka kumi.

Akiwa katika Gereza la Wha Wha, baadaye Sikombela kisha Salisbury, alifanikiwa kuhitimu digrii mbili za sheria; BSC Bachelor of Law na MSC Master of Law kutoka Chuo Kikuu cha Uingereza, progamu za nje

STORI: ERICK EVARIST, DAR

Comments are closed.