Utamu wa Tamthiliya ya Mke Mtemi ya Global TV
MAMBO ni motooo! Ndivyo unavyoweza kusema ikiwa ni siku chache baada ya Tamthiliya ya Mke Mtemi ya Global TV kuachiwa rasmi na kuteka mioyo ya mashabiki wengi.
Umeshajua utamu wa tamthiliya hii? Kama bado basi jua unakosa mengi kwani ni zaidi ya tamthiliya uliyowahi kuiona. Iko hivi;
Mke Mtemi ni tamthiliya ya vichekesho makini (serious comedy) yenye mtazamo tofauti katika jamii ambapo imejikita katika kufichua na kuonesha changamoto wanazokutana nazo wanaume katika ndoa zao.
Mhusika mkuu katika tamthiliya hiyo ni binti aitwaye Shenaiza ambaye ameolewa na kijana mmoja kijijini kwao aitwaye Hemed lakini maisha yao ya ndoa yamekuwa na misukosuko mingi, mwanamke akimnyanyasa sana mumewe na kumshushia kichapo mara kwa mara.
Hali hiyo inasababisha jamii kuingilia kati kutaka kumsaidia kijana huyo lakini Hemed anakataa kuonesha ushirikiano kwa kuficha matatizo kwa hofu ya kipigo, huku akisema kwamba anaishi vizuri na mkewe.
Mama mzazi wa Hemed pamoja na mjomba wake wanaona njia ya kumsaidia kijana wao ni kwenda kwa mganga lakini mwisho hali ndio inazidi kuwa mbaya.
Shenaiza anazidi kumfanyia mumewe vituko, maisha ya Hemed yanakuwa ya kuteswa na kunyanyaswa kila kukicha mpaka kukosa rafiki au jirani wa kumsadia, na baada ya manyanyaso kuzidi, tukio kubwa na baya zaidi linatokea.
Je, ni tukio gani hilo? Nini mwisho wa wanandoa hawa? Kupata uhondo kamili, usikose kutazama tamthiliya hii inayorushwa kila siku kupitia Global TV.
Namna ya kutazama, ingia katika simu yako, laptop au kompyuta, nenda Youtube kisha andika Global TV, bofya alama nyekundu yenye maneno SUBSCRIBE kisha endelea kufaidi uhondo.
Risasi Vibes.
Comments are closed.