Utasikitika Kwa Maamuzi Aliyoyachukua Tajiri Namba Moja Duniani Na Mkewe

 

MMILIKI na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Amazon, Jeff Bezos,  na mkewe MacKenzie wanatarajiwa kupeana talaka baada ya miaka 25 ya ndoa.

 

Wawili hao wametoa taarifa ya pamoja kuhusu suala hilo kupitia mtandao wa Twitter siku ya Jumatano Januari 9 mwaka huu.

 

 

 

“Baada ya kipindi kirefu cha mapenzi na kujaribu kutengana, tumeamua kuachana na kuendelea na maisha yetu kama marafiki,” wawili hao wamesema kwenye taarifa yao ya pamoja.

 

Amazon, ambayo imeanzishwa miaka 25 iliyopita wiki hii imeifunika Microsoft na kuwa kampuni yenye thamani kubwa zaidi duniani.

 

Amazon ina thamani ya Sola bilioni 797 baada ya soko la hisa la Marekani kufungwa siku ya Jumatatu kufuatia kukua kwa asilimia 3.4,  ikiipiku Microsoft ya Bill Gates yenye thamani ya Dola bilioni 789.

 

Bezos, 54, ambaye ni mwanzilishi wa Amazon, ndiye mtu tajiri zaidi ulimwenguni kwa mujibu wa chati ya jarida mashuhuri la biashara la Bloomberg, akiwa na utajiri unaokisiwa kufikia Dola bilioni 137, akimzidi Bill Gates kwa Dola bilioni 45.

 

Bi MacKenzie Bezos mwenye miaka 48 ni mtunzi wa vitabu, na baadhi ya maandiko yake ni The Testing of Luther Albright (2005) na Traps (2013).

“Tunajihisi ni wenye bahati kwa kufahamiana na tunafurahia miaka yote tuliyokuwa pamoja kwenye ndoa,” taarifa ya wawili hao imeeleza.

 

 

“Laiti tungelijua kama tungetengana baada ya miaka 25, basi tungelianza upya. Tumekuwa na maisha bora kabisa kama wanandoa na pia tunaona mustakabali mzuri kama wazazi, marafiki na washirika katika miradi na biashara mbalimbali.

 

“Japo nembo zitabadilika, tutabaki kuwa familia, na tutaendelea kuwa marafiki wa kipekee.”

 

Mwaka jana walianzisha kwa pamoja wakfu uitwao Day One Fund unaolenga kuwasaidia watu wasiokuwa na makao pamoja na kujenga shule za awali kwenye maeneo waishio watu wenye vipato duni.

 

Wawili hao wana watoto wanne – wavulana watatu na binti mmoja ambaye wamemuasili.

 

Vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti kuwa  Bezos yupo kwenye dimbi la mahaba na mtangazji wa zamani wa runinga ya Fox TV, Bi Lauren Sanchez.

 

Mtandao wa habari za burudani wa TMZ, ukinukuu vyanzo vilivyo karibu na Bi Ms Sánchez, unadai kuwa wawili hao wamekuwa kwenye mapenzi mpaka mwisho wa mwaka jana.

 

Mwaka 2013, MacKenzie Bezos aliliambia jarida la Vogue kuwa alikutana na Jeff wakati akimfanyia usaili wa kazi katika wakfu wa Hedge jijini New York.

 

Wawili hao waliingia katika uchumba miezi mitatu tu toka walipoanza mahusiano na kufunga ndoa muda mfupi baadaye mnamo mwaka 1993.

 

Mwaka mmoja baadae Jeff akaanzisha Amazon –  kampuni ya kuuza vitabu reja reja mtandaoni.

 

Kampuni hiyo imekua toka hapo na kuwa gwiji nambari moja wa biashara ya mtandao duniani.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

 

Loading...

Toa comment