Utata Kifo Francis Cheka: Mkewe Afunguka Kila Kitu – Video

Siku chache zilizopita ulizuka uvumi wa kwamba bondia, Francis Cheka, amefariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro baada ya lori la mafuta kulipuka na kuua zaidi ya watu 70.

 

Ilisemekana kwamba Francis Cheka ambaye anaishi mkoani humo na anafanya biashara zake maeneo ya Msamvu ambapo ajali ilitokea, kuwa siku ya tukio alikuwepo ofisini kwake na lori lilivyolipuka likaondoka na maisha yake.

 

Katika kuthibitisha taarifa hizo, Global TV imefanya jitihada za kumtafuta mke wa Francis Cheka, ambaye amekanusha taarifa hizo na kusema mumewe yupo hai.

 


Loading...

Toa comment