The House of Favourite Newspapers

Utawaambia Nini Wakazi wa Jimbo la Kibiti na Twaha Mpembenwe Wao?

0

 

Wakazi wa Mjawa akimpongeza Twaha Mpembenwe baada ya kumaliza mkutano.

Pwani, 11 Januari 2023: Utawaambia nini wakazi wa Kibiti na Twaha Mpembenwe wao mwenye kauli mbiu ya “Kibiti kwa Maendeleo”?

Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kwa jinsi wakazi Jimbo la Kibiti mkoani Pwani furaha waliyonayo kwa mbunge wao, Twaha Mpembenwe kutoka Chama cha Mapinduzi aliyeingia madarakati katika uchaguzi mkuu wa 2020.

Wakazi wa Mwera Magharibi wakipongeza mbunge wao Mpembenwe kwa mambo mbalimbali kijijini hapo.

Mbunge huyo ambaye anasifika kwa kuboresha jimbo hilo pamoja na kuinua uhai wa CCM jimboni humo akishirikiana na wafadhili alionao ameweza kufanikisha ukarabati wa ofisi za CCM na majengo ya huduma za jamii.

Kinamama wa Kijiji cha Mjawa Jimbo la Kibiti wakiwa na kanga inayomuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kumuunga mkono kwa maendeleo ya kasi yanayoonekana kjijini kwao kupitia mbunge wao.

Mpembenwe amefanikiwa kupeleka shehena kadhaa za nondo, saruji na mabati kutoka kwa wahisani wake ikiwemo Kampuni ya PMM Estate (2001) LTD inayojishughulisha na utoaji wa mizigo bandarini na wengineo.

Pamoja na kufanikisha hayo, Mpembenwe amekuwa akimshukuru mara kwa mara Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuwezesha kufanikisha maendeleo ya kasi ya jimbo hilo.

Mbunge Mpembenwe alipomtembelea mmoja wa wazee wasiojiweza wakati akielekea kwenye ziara yake kijiji cha Kiongoroni.

Baadhi ya majengo ya huduma za kijamii aliyoyaboresha mbunge huyo ni pamoja na zahanati na shule za msingi na sekondari.

Hivi karibuni mbunge huyo kupitia wafadhili wake ameweza kuikarabati ofisi ya Chama cha Mapinduzi ya Wilaya hiyo na kujenga flemu nane za kisasa ambazo zitatumika kama kitega uchumi kwa kuwapangisha wawekezaji.

Mbunge Mpembenwe (nyuma mwenye kofia nyeupe) na baadhi ya wanachama wa CCM wakivuka kwa mtumbwi kuelekea kijiji cha Kiongoroni kuzungumza na wananchi.

Jengo hilo pia lina ukumbi unaochukua watu zaidi ya 1500 ambapo hata uchaguzi wa viongozi CCM Wilaya hiyo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana ulifanyika ukumbini humo kwa wanachama kujifungia kwenye ukumbi huo na kufanya uchaguzi wao kistaarabu na amani kabisa.

Mpembenwe tofauti na wabunge wengine wanaowasahau wapiga kura wao baada ya kupitishwa kwenye uchaguzi yeye amekuwa akifanya ziara mara kadha wa kadha kwa wananchi wake kuwajulia hali, kubadilishana nao mawazo na kujadiliana changamoto za maeneo yao.

Mbunge Mpembenwe alipokuwa akizungumza na wananchi jimboni Kibiti.

Mwishoni mwa mwaka jana alifanya ziara ya kuwashukuru wananchi wake kwa kumuingiza madarakani na kujadiliana nao changamoto mbalimbali katika maeneo yao.

Baadhi ya vijiji alivyopita ni pamoja na Mjawa, Mtawanya, Mbwera Magharibi, Mbuchi na kisiwa cha Kiongoroni ambapo baadhi ya vijiji vimekuwa na changamoto ya ufikaji lakini yeye alifika kama wanavyofika wengine.

 

Mmoja wa wanachama wa upinzani akirudisha kadi kwa viongozi walioambatana na mbunge Mpembenwe kwenye ziara yake.

Kutokana na baadhi ya mambo aliyoyafanya wakazi wengi wa jimbo hilo wamekuwa wakimuona kama mkombozi wao kufikia hata wengine kumpa zawadi mbalimbali kama vile kuku na nyinginezo.

Katika ziara zake zote ambazo wanahabari wetu walihudhuria walishuhudia makundi ya wanachama kutoka vyama vya upindani wamekuwa wakirudisha kadi zao na kujiunga na CCM katika jitihada za kumuunga mkono mbunge huyo.

Waliokuwa wanachama kutoka upinzani kwenye moja ya vijiji wakionesha kadi za CCM baada ya kurudisha kadi za vyama vyao na kupewa za CCM.

Huyu ndiye Mbunge wa Jimbo la Kibiti Twaha Mpembenwe mwenye kauli ya “Kibiti kwa Maendeleo Inawezekana”.

MAKALA HII IMEANDALIWA NA RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY WA GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply