The House of Favourite Newspapers

Utoaji wa Malalamiko na Kero Juu ya Huduma za Afya Nchini

2.Kaimu Mkurugenzi wa Kinga Dkt.Khalid Massa (katikati) akifafanua jambo.Kaimu Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Khalid Massa (katikati) akifafanua jambo. 3.Ummy (katikati) akisikiliza maswali ya wanahabari yaliyokuwa yakiulizwa baada ya taarifa yake.Ummy (katikati) akisikiliza maswali ya wanahabari yaliyokuwa yakiulizwa baada ya taarifa yake. 4. ..Akienelea kufafanua jambo.…Akienelea kufafanua jambo.

ummy afyaUTOAJI WA MALALAMIKO NA KERO JUU YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI PAMOJA NA MASUALA YA JINSIA, WAZEE NA WATOTO

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayo dhamana ya kusimamia na kuratibu Mipango, Sera, Sheria na Mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini pamoja na kujenga jamii ya watanzania inayojali na kuheshimu Usawa wa Jinsia, Haki za Wazee na Watoto.

Katika utekelezaji huu, yapo mafanikio kadhaa yaliyopatikana lakini pia zipo changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utoaji wa huduma za afya hapa nchini. Baadhi ya changomoto hizo ni za kiutendaji zaidi ambazo zinaweza kutatuliwa kwa haraka endapo tutaimarisha usimamizi na uwajibikaji katika kila ngazi kuanzia ngazi ya Wizara, Mikoa, Wilaya na Vituo vya kutolea huduma za afya. Changamoto hizi ni pamoja na wagonjwa kutopatiwa huduma haraka na sahihi, lugha na kauli mbaya kutoka kwa watoa huduma na makundi yanayotakiwa kupata matibabu bure (yaani Wazee, Wajawazito na Watoto wa umri wa chini ya miaka 5) kutozwa fedha kinyume na Sera ya Afya ya 2007). Takribani kila siku vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti matukio kadhaa kuhusu malalamiko na kero mbalimbali wanazokumbana nazo wananchi  katika kupata huduma za afya.

Wasimamizi wa Wakuu wa Utekelezaji wa Sera na Miongozo ya Afya katika ngazi ya Mikoa ni Waganga Wakuu wa Mikoa. Ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya pamoja na kuhakikisha malalamiko na kero zao zinashughuhulikiwa kwa haraka, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) ameamua kuweka wazi namba za simu za Waganga Wakuu wa Mikoa (RMO) wote nchini ili wananchi wanapokuwa na malalamiko/kero waweze kuwasiliana nao moja kwa moja. Mhe Waziri amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa kuyafanyia kazi masuala yote yanayoletwa na wananchi katika Mikoa yao na kuyapatia ufumbuzi haraka. Hivyo, wananchi wasisite kuwasiliana nao kupitia namba zao zifuatazo pamoja na kwa barua pepe.

Katika muktadha mzima wa kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa Sheria na Sera za Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini, mwananchi yoyote ambae ana malalamiko, maoni au ushauri kuhusu sekta husika unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (Mb) kupitia simu namba 0746 – 505030 (kwa njia ya ujumbe) pamoja na kueleza mkoa uliopo, twitter @wamjw na email: [email protected]

“Uwazi na Uwajibikaji ni chachu ya kuleta mabadiliko katika sekta ya afya, sambamba na kulinda Haki za Watoto, Wazee na Wanawake”.

Imetolewa na:

Nsachris Mwamwaja

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

22/08/2016

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

MAWASILIANO NA WAGANGA WAKUU WA MIKOA (RMOs)

NA. MKOA JINA LA MGANGA MKUU NAMBA YA SIMU NUKUSHI
1. ARUSHA DKT. FRIDA MOKITI 0784-264750 [email protected].
2. DAR ES SALAAM DKT. GRACE MAGEMBE 0767-300234 [email protected]
3. DODOMA DKT. JAMES CHALRES 0784-504955 [email protected]
4. IRINGA DKT. ROBERT M. SALIM 0754-377176 [email protected]
5. KAGERA DKT. THOMAS RUTACHUNZIBWA 0754-803729 [email protected]
6. KIGOMA DKT. PAUL CHAOTE 0755-696855 [email protected]
7. KILIMANJARO DKT. BEST MAGOMA 0754-621046  
8. LINDI DKT. SONDA YUSUPH 0653-384350 [email protected]
9. MANYARA DKT. SUNGWA KABISSI NDAGABWENE 0713-450765 [email protected]
10. MARA DKT. SAMSON WINANI 0784-450425 [email protected]
11. MBEYA DKT. SEIF MHINA 0767-832275 [email protected]
12. MOROGORO DKT. JACOB FRANK 0767-985850  
13. MTWARA DKT. WEDSON SICHALWE 0755-048787  
14. MWANZA DKT. LEONARD SUBI 0784-501020 [email protected]
15. PWANI DKT. BEATRICE BYARUGABA 0784-319764 [email protected]
16. RUKWA DKT. JOHN GURISHA 0784-216008 [email protected]
17. RUVUMA DKT. DAMAS KAYERA 0713-537495 [email protected]
18. SHINYANGA DKT. NTULI KAPOLOGWE 0654-586346 [email protected]
19. SIMIYU DKT. MAGEDA KIHULYA 0754-507875 [email protected]
20. SINGIDA DKT. JOHN MWOMBEKI 0786-103225 [email protected]
21. TABORA DKT. GUNINI KAMBA 0783-344079 [email protected]
22. TANGA DKT. ASHA MAHITA 0715-465521 [email protected]
23. GEITA DKT. JOSEPH KISALA 0788-046787 [email protected]
24. KATAVI DKT. YAHYA HUSSEIN 0754-372772 hyahaya70yahoo.com
25. NJOMBE DKT. SAMUEL MGEMA 0757-226806 [email protected]

 

IMETOLEWA TAREHE 22/08/2016