The House of Favourite Newspapers

Uturuki yaitungua ndege ya Urusi

0

Turkish (2) Ndege hiyo ikiteketea angani mara baada ya kutunguliwa.Turkey (1)Ndege hiyo ikiteketea angani mara baada ya kutunguliwa.Turkey (2)Rubani akishuka kwa parachuti.possible pilot of downed Russian jet over Turkey Identity unconfirmed

Rubani mmoja amekutwa amekufa.Turkey (4)Vifaa kwa ajili ya huduma ya kwanza alivyokutwa navyo rubani aliyefarikiTurkish (5) Ikiwa inadondoka chini.Turkish (4)Marubani wakishuka kwa parachuti.Turkish (3) …Ikidondpka.
Turkish (1)

Moshi mkubwa.

JESHI la Uturuki kwa kutumia ndege zake za kivita F-16, limeitungua na kuilipua ndege ya kivita ya Urusi aina ya Sukhoi Su-24, karibu na mpaka wake na nchi ya Syria leo asubuhi, Ankara na Moscow zimethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo.

Maofisa wa Usalama nchini Uturuki wamesema kuwa, Jeshi lao limeamua kuchukua hatua hiyo baada ya agizo lao la mara kwa mara kuitaka Urusi isipitishe ndege zake za kivita kwenye anga la Uturuki karibu na mpaka wa Syria, japo Urusi wamekaidi agizo hilo.

Kwa upande wake, Jeshi la Ulinzi nchini Urusi wajitetea kuwa ndege yao haikuwa kwenye anga la Uturuki bali ilikuwa kwenye anga la Syria wakati Waturuki wakiishambulia.

Vyombo vya habari vya Utruruki vimesema kuwa, vimenasa picha zikionesha marubani wawili wakiruka kwa parachute na kuokoka wakati ndege hiyo ikiteketea angani kabla ya kutua ambapo dakika tano baadae walipofika eneo la tukio walikuta mwili wa rubani mmoja akiwa tayari amefariki dunia.

Leave A Reply