UVCCM Yawapiga Tafu Wanachuo Kupata Mkopo Elimu ya Juu – Video

Mwanaidi Kipingu akielezea jinsi wanafunzi  wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu wanavyoweza kupata mikopo  kiurahisi na kuwataka wawahi kufika kwenye ofisi husika za mikopo (HESLB).

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeanzisha mpango wa kuwasaidia wanachuo wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu jinsi ya kujaza fomu na kuomba mkopo kupitia Bodi ya Mikopo ya kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Wanafunzi waliojitokeza wakisaidiwa kujaza fomu za kuombea mikopo hiyo.

Akizungumza na mwandishi wetu, ofisa wa UVCCM, Mwanaidi Kipingu, amesema msaada huo wanautoa bila kuangalia itikadi za kisiasa wala zozote zile.

Mwanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Elius Lungwa, akieleza alivyohangaika muda mrefu kupata mkopo wa kumwendeleza kielimu na kumaliza shida hiyo kiurahisi baada ya kufika kwenye ofisi za HESLB.

Aidha amewataka wanafunzi wote wanaohitaji kuomba mikopo hiyo wajitokeze mapema katika ofisi za UVCCM zilizopo makutano ya Barabara ya Morogoro na Lumumba Dar es Salaam.

 Mwanafunzi Mwamvua Hussein ambaye alimaliza diploma na kufika ofisi hizo kwa ajili ya mkopo wa kumwezesha kusoma digrii akishukuru baada ya kukamilisha mchakato huo

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

Loading...

Toa comment