The House of Favourite Newspapers

Uvimbe katika kizazi cha mwanamke-2

0

wherefibroidsgrowWiki iliyopita tulianza kupeana elimu ya uvimbe unaoota katika kizazi cha mwanamke. Pamoja na kuwa kumekuwa na uvimbe mbalimbali katika kizazi cha mwanamke tulianza na faibroids au mayoma.

Tuliangalia chanzo pamoja na maana ya uvimbe huo. Leo ningependa tupeane ufahamu kuhusu aina na dalili za kutambua kuwa mwanamke husika ana tatizo hili la uvimbe unaoota katika kizazi. Wanawake wengi wamekuwa wakilalamika wanasumbuliwa na tatizo hili la uvimbe kwenye kizazi.

Kama msomaji umekwenda hospitali na ukaambiwa una tatizo hilo usipate shaka mbali na kufanyiwa upasuaji kuna mimea na matunda tiba ambayo yanaweza kuondosha tatizo lako na ukarejea katika hali yako ya kawaida kabisa.

Unaweza ukatembelea Sigwa Herbal Clinic iliyopo Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Arusha, Dodoma  na Kahama kwa uchunguzi na matibabu.

Aina za uvimbe wa fibroid.

Fibroid zinatofautishwa kutokana na sehemu ilipotokea. Zipo zinazotokea ndani ya mji wa mimba na nyingine zinatokea kwenye kuta za nje ya mji wa mimba. Msomaji tambua kuwa karibu asilimia 75 ya wanawake wenye fibroid hawajui kama wana tatizo hilo. Si rahisi mtu kuona dalili na kutambua mara moja kuwa ana tatizo la fibroids.

Utambuzi wa dalili za fibroid hutegemea ukubwa wake na mahali zilipo kwenye kizazi. Hii pia huchangiwa na dalili anazopata mgojwa husika. Eneo ambalo fibroid imeota ndiyo huamua dalili husika. Kwa mfano:  Fibroid kubwa inayoota nje ya kizazi haitakuwa na dalili sawa na fibroid ndogo iliyo kwenye kuta za kizazi.

Baadhi ya aina hizo ni kama vile; unaotokea ndani ya kizazi, unaotokea katikati ya misuli ya kizazi na unaotokea nje ya kizazi.

Uvimbe huu pia unaweza kuchomoza katika mdomo wa kizazi au ukaning’inia ndani au nje ya kizazi.

Dalili za fibroid

Dalili kubwa inayofahamika zaidi ni ile ya kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi na  maumivu ya tumbo. Damu hii hutoka kidogokidogo kwa muda mrefu kuliko ulivyozoea mzunguko wako.

Pia huathiri mfumo wa haja ndogo na kubwa, na mgonjwa kuhisi mkojo mara kwa mara, mkojo kutoka kidogokidogo, kushindwa kutoka kirahisi, kukosa choo.

Maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Fibroid zaweza kusababisha matatizo kama kuharibu mimba au mwanamke kutoshika mimba kutokana na mirija ya uzazi kubanwa au msukumo unaosababishwa na fibroid, mirija ya uzazi hubanwa na hivyo kushindwa kupitisha mayai kuelekea kwenye kizazi (uterus).

Mwanamke anapokuwa mjamzito pia akawa na fibroid, mwili huweza kusitisha kupeleka damu kwenye fibroid na kuifanya isinyae hivyo kusababisha maumivu makali ya tumbo na kufanya kizazi kutanuka na kusinyaa na baadaye mimba huweza kutoka kabla ya wakati wake.

Wakati wa kujifungua, kama fibroid itakuwa kwenye njia ya kutolea mtoto inaweza kusababisha damu nyingi kutoka au ikishindikana, mama hufanyiwa upasuaji ili kumtoa mtoto aliye tumboni.

Mzunguko wa hedhi unavurugika kiasi kwamba  hujui siku zako ni lini na uwezo wa kushika mimba unapotea.

Hali inaweza kuendelea hivyo na ukajikuta unaishiwa damu na mwili unakuwa dhaifu.

Itaendelea wiki ijayo!

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Leave A Reply