The House of Favourite Newspapers

Uvimbe katika kizazi cha mwanamke-3

0

maumivuKAMA tulivyokuwa tukipeana elimu ya afya zetu wiki zilizopita, wiki hii pia ni mwendelezo wa mada ya uvimbe katika kizazi cha mwanamke.

Leo ningependa tuendelee na athari za uvimbe huo katika afya ya mwanamke.

Mara nyingi mwanamke anagundulika na tatizo la fibroid kama ataenda hospitali kwa lengo la kutafuta ujauzito. Niwakumbushe wasomaji kuwa, kama unaona una  maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa muda mrefu, maumivu wakati wa tendo la ndoa, kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi tambua kuwa hiyo si hali ya kawaida na haiwezi kuondoka yenyewe bila kufanya matibabu. Ni vema ukawahi kufanyiwa uchunguzi ili kubaini tatizo.

Athari za uvimbe

Kwanza kabisa uvimbe huu  unakua mkubwa na kukusababishia maumivu. Mwanamke mwenye uvimbe huu hupata maumivu makali chini ya kitovu lakini pia maumivu ya kiuno na mgongo.

Pia uvimbe huu ukiota katika kizazi cha mwanamke unaweza kusababisha mwanamke asipate ujauzito kabisa.

Pia uvimbe huu unaweza kusababisha mimba kuharibika. Uvimbe ukiwa katika misuli ya kizazi unasababisha  mimba isikue na  baadaye ikatoka.

Uvimbe ukiwa nje ya kizazi athari zake ni kupata maumivu makali sana wakati wa ujauzito na ukajikuta mimba inatoka au itakubidi uzae kwa upasuaji.

Athari kubwa nyingine ya uvimbe upasuaji wake ni wa kuondoa kizazi kwa kuwa kunakuwa hakuna jinsi. Kwa hiyo unajikuta huna mtoto na umechelewa kutibiwa na uvimbe umekua mkubwa hivyo huna budi kuondolewa kizazi.

Uvimbe wa fibroid usipodhibitiwa unakua mkubwa sana kwa haraka, ukuaji wake unategemea kiwango kikubwa cha homoni ya estrogen mwilini.

Lakini mwanamke mwenye uvimbe katika kizazi chake anaweza akakumbwa na tatizo la kupata choo kwa shida. Hii ni kutokana na uvimbe unavyozidi kuongezeka unaenda kuminya njia ya haja kubwa na kusababisha tatizo la kupata haja kubwa kwa shida.

Matibabu na ushauri.

Tiba hufanyika baada ya uchunguzi wa kina kuona kama uvimbe upo vipi na una ukubwa gani. Uvimbe mdogo unaweza kutibika kwa dawa huku mwanamke akipewa msisitizo abebe ujauzito, uvimbe mkubwa lazima upasuaji ufanyike. Lakini pia niwatoe hofu wasomaji kuwa ikiwa umekwenda hospitali na ukaambiwa una uvimbe kwenye kizazi unaweza ukatembelea Sigwa Herbal Clinic kwani ni wataalamu wana mimea tiba ambayo inaweza kuyeyusha uvimbe wa aina zote bila kufanya upasuaji.

Ni vema ukafuatilia makala haya ili kupata elimu zaidi na  nikukumbushe kuwa Sigwa Herbal Clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume unaweza ukawatembelea katika vituo vyao. Bukoba, Njombe, Singida, Dar es Salaam, Moshi, Tanga, Mwanza, Mbeya, Arusha, Kahama, Kigoma, Dodoma na Morogoro.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Leave A Reply