Uvimbe katika kizazi cha mwanamke

uvimbeBAADA ya kupeana elimu juu ya tatizo la uvimbe kwenye ovari. Leo ningependa tupeane ufahamu kuhusu uvimbe unaoota katika kizazi cha mwanamke.

Wanawake wengi wamekuwa wakilalamika wanasumbuliwa na tatizo hili la uvimbe kwenye kizazi. Hii ni baada ya kufanyiwa uchunguzi katika hospitali mbalimbali. Wanawake wamekuwa wakigunduliwa na uvimbe mbalimbali katika mfumo wao wa uzazi.

Leo ningependa kuanza na uvimbe unaoota katika kizazi unaitwa Fibroid kwa kitaalam.

Fibroid ni uvimbe unaoota ndani ya kizazi cha mwanamke, ambapo hutengenezwa na kambakamba zilizofungamana yaani muscle fibre na uvimbe huu upo kama nyama laini.  Nikukumbushe kuwa suala hili linawasumbua wanawake wengi sana na limeweka mshtuko mkubwa katika jamii. Kuna mitazamo mingi juu ya suala hili kuna wenye imani kwamba mwanamke akikumbwa na tatizo hii huenda karogwa. Kuna wengine hawajui lolote wanaliona kama ni tatizo ambalo limeanza hivi karibuni.

Pia takwimu huonesha kuwa tatizo hili pia huwapata zaidi wanawake wa Kiafrika kuliko Wazungu, yaani maeneo ya Afrika, India na Amerika. Vilevile tatizo huwatokea zaidi wanawake ambao hawajashika ujauzito au hawajawahi kuzaa kabisa hadi wanapofikia umri wa kati, kuanzia miaka 28 na kuendelea.

Wanawake ambao wameshazaa hupatwa na tatizo hili lakini mara chache kulinganisha na wale ambao hawajazaa kabisa au walishazaa mtoto mmoja au wawili na wakakaa muda mrefu  bila ya kuzaa, nao hukabiliwa na tatizo hili.

Fuatilia makala haya kupata uelewa mzuri juu ya tatizo hili linalosumbua jamii yetu kwa kiasi kikubwa kwa sasa.

Chanzo cha tatizo?

Chanzo halisi cha aina hii ya uvimbe bado hakijulikani lakini ni tatizo linalosumbua zaidi wanawake walio katika umri wa kuzaa. Umri wa mwisho kuzaa ni kuanzia miaka arobaini na tano na kuendelea hadi hamsini.

Kama tulivyoelezea hapo juu, chanzo halisi hakijulikani, yaani huwa inatokea tu kutokana na mabadiliko ya mwili wa mwanamke, mabadiliko haya yanahusisha mfumo wa homoni wa mwanamke pamoja na chembe hai za kizazi.

Mara nyingi fibroid hukua kwa mwanamke pale kiwango cha ‘oestrogen’ kinapoongezeka mwilini pia fibroid hupungua wakati kiwango cha ‘oestrogen’ nacho kikipungua.

Oestrogen ni mkusanyiko wa homoni ambazo ndizo zinazoukuza mwili wa mwanamke kijinsia. Mfano ni ukuaji wa viungo kama matiti na kupata hedhi.

Kama msomaji umekwenda hospitali na ukaambiwa una tatizo hilo usipate shaka mbali na kufanyiwa upasuaji kuna mimea na matunda tiba ambayo yanaweza kuondosha tatizo lako na ukarejea katika hali yako ya kawaida kabisa.

Baada ya kuangalia utangulizi wa mada yetu nzuri nikukumbushe kuwa Sigwa Herbal Clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume unaweza ukawatembelea katika vituo vyao. Njombe, Singida, Dar es Salaam, Moshi, Tanga, Mwanza, Mbeya, Arusha, Kahama, Kigoma, Dodoma na Morogoro.


Loading...

Toa comment