Uvumilivu Wamshinda Esma

ESMA Khan au Esma Platnumz, dada wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema kuwa anakubali watu waendelee kumuita Yuda kwa sababu hawezi kuvumilia kufanyiwa mambo yasiyoeleweka halafu akanyamaza, eti kisa anaogopa kuitwa Yuda.

 

Esma alipewa jina la Yuda likiwa na maana ya msaliti kufuatia tabia yake ya kuwageuka wanawake wanakuwa na Diamond kimapenzi. Esma ameiambia ShowBiz kuwa, siku zote watu wa nje ya familia yao hawawezi kujua mambo ya ndani kwao hivyo bora wangenyamaza

 

“Kiukweli uvumilivu umenishinda. Wanaoniita Yuda waendelee tu maana vitu vingine si vya kuvumilia hata kidogo na siku wasiponiita Yuda, ujue kabisa aliyekuja kwetu (mwanamke wa Diamond) hana tatizo lolote,” alisema Esma.

 

Esma aliyasema hayo baada watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii kumtaja kuwa ndiye chanzo kuvurugika kwa uhusiano wa kaka yake na wapenzi wake.

STORI: IMELDA MTEMA

 

SHABIKI WA YANGA Awatahadharisha SIMBA “Msije na PAWA BENKI” Kigelegele

Toa comment