The House of Favourite Newspapers

Uwazi Lapasua Anga Vikindu, Kongowe

0

UWAZI (1)

Mzee Makarani Shaweji mkazi wa Vikindu akisoma Gazeti la Uwazi.

UWAZI (2)

Fundi Mwinyi Chande akisoma Uwazi, pembeni ni muuzaji wa gazeti hilo, Mwamvita Rashid.

UWAZI (3)

Abdallah Mgeni akilisoma Uwazi ofisini kwake maeneo ya Vikindu.

UWAZI (4)

Nyanyige Maguri mkazi wa Kongowe akiwa akisoma kwa makini Gazeti la Uwazi.

UWAZI (5)

Kaburu mkazi wa Kongowe akisoma Uwazi akiwa sambamba na Ofisa Usambazaji, Jimmy Haroub (kushoto).

GAZETI la Uwazi linazidi kupasua anga kutokana na wasomaji wake kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar kujipatia nakala zao kila Jumanne linapotoka ikiwa ni baada ya kufikishiwa pale wanapoishi.

Leo wauzaji wa Gazeti la Uwazi pamoja maofisa usambazaji walitembelea mitaa ya Vikindu, Kongowe na maeneo mengine wakiuza gazeti hilo lililosheheni habari za kusisimua ambapo wasomaji wengi walionyesha kulifurahia na kuchangamka kulinunua.

Akizungumza, msomaji aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Mgeni mkazi wa Vikindu alisema anavutiwa sana na habari zinazochapishwa kwenye Gazeti la Uwazi kwani ni za kina, zinasisimua na zinaelimisha jamii kwa jumla.

“Kiukweli nalipenda sana gazeti la Uwazi kwa sababu habari zake ni  tofauti huwezi kuzipata kwenye gazeti lingine lolote, pia zinaandikwa kiundani na zinasisimua, nawaomba na wengine walinunue nawalisome,” alisema Abdallah.

PICHA/STORI NA GLADNESS MALLYA/GPL

Leave A Reply