The House of Favourite Newspapers

UWOYA ACHARUKA ISHU YA KUBADILI DINI

Irene Uwoya

TOFAUTI na wengi wanavyoamini kwamba muigizaji Irene Uwoya ni Muislamu na aliuacha Ukristo baada ya kuolewa na bwa’ mdogo Dogo Janja (Abdulaziz Chende), mrembo huyo ameibuka na kusema hajawahi kubadili dini yake ya awali.  

 

Uwoya alisema kwa muda mrefu amekuwa akisema kuwa hawezi kubadili dini yake ya Kikristo hivyo watu wafahamu kuwa yeye ni Mkristo na waondoe dhana kwamba alikuwa dini nyingine tofauti.

 

“Nawashangaa sana watu kila kukicha wananiuliza umerudi kwenye dini yako ya awali kama kuna siku hata moja nilishawahi kuwaambia kuwa nimebadilisha dini yangu ya Kikristo yaani siwezi na sijawahi kujaribu,” alisema Uwoya licha ya kuwa inafahamika alifunga ndoa halali ya Kiislamu na Dogo Janja kabla hawajamwagana hivi karibuni.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Comments are closed.