UWOYA amfanyia mbaya Johari

ZANZIBAR: Staa mkubwa wa filamu Bongo, Irene Uwoya amemfanyia kitu mbaya mwigizaji mwenzake, Blandina Chagula ‘Johari’.  Uwoya amemshtukiza Johari ambaye ni shoga’ke mkubwa na kummwagia ndoo za maji kwenye kumbukumbu yake ya kuzaliwa kiasi cha kumfanya apagawe. Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na Gazeti la Ijumaa visiwani Zanzibar, hivi karibuni, ishu hiyo ilikuwa hivi; Johari alikuwa kwenye pilikapilika za hapa pale za

kuandaa chakula ambacho kilikuwa maalum kwa ajili ya sherehe iliyoandalia na uongozi wa Kampuni ya Swahiliflix wakati wakiwa kambini visiwani Zanzibar.

Wakati Johari akiwa hajui hili wale lile, Uwoya alikuwa akihesabu saa na ilipotimia saa sita na dakika moja usiku, alichukua ndoo kubwa iliyojaa maji kisha akammwagia Johari kwa nyuma, jambo ambalo lilimshtua mno mwanadada huyo na kuanza kukimbia huku na kule na baadhi ya mastaa wengine wakimkimbiza na kummwagia maji na pombe.

Baada ya kuona anashambuliwa na maji huku Uwoya akiendelea kummwagia maji, Johari alianza kuangua kilio huku akisema Uwoya hakumtendea haki. “Jamani hii siyo haki kabisa, hapa mngeniua mwenzenu kwa sababu mimi nilishajisahau kama mnaweza kunifanya hivyo yaani mngekuta presha yangu iko juu mngeniua,” alisema Johari ambaye alilazimika ya kwenda kubadili nguo. Hata hivyo, hata baada ya jambo hilo kumalizika, bado Johari alionekana mwenye huzuni.


Loading...

Toa comment