The House of Favourite Newspapers

Uwoya Anammisi Masogange Kinoma

STAA wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya anammisi kinoma aliyekuwa rafiki yake, marehemu Agness Gerald ‘Masogange’ na anatamani angekuwepo.

 

Uwoya aliiambia Shusha Pumzi kuwa, kutokana na ukaribu waliokuwa nao amekuwa akimisi mno uwepo wa Masogange, lakini hana jinsi kwa sababu ni kazi ya Mungu.

 

“Siyo siri, ninammisi kinoma Masogange ndiyo maana eneo tulilokuwa tukiishi mwanzo nilihama na sikutaka tena kuishi mitaa hiyo kwa sababu Masogange alikuwa akinitokea sana, nikawa nahisi kama yupo hai, mwisho nikaona bora nihame ili nisahau, lakini bado ninamkumbuka mno,” alisema Uwoya.

STORI: IMELDA MTEMA

Comments are closed.