The House of Favourite Newspapers

Uwoya Ashangaa Kupewa Makavu Insta!

Staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya.

STAA wa filamu Bongo, Irene Uwoya, amewafungukia watumiaji wa Instagram wanaokosoa vazi lake la ufukweni.

Mrembo huyo ambaye ni mke wa msanii Dogo Janja amesema yeye si wa kwanza kufanya hivyo.

Uwoya ameandika katika Instagram:

Ukivaaa nguo kawaida anakigodoro, nikimpost mume ooh mdogo, nisipo post kwanini humpost humpendi. Nikivaaa nguo za ufukweni nipo uchi mke wa mtu.

Sasa nasema hivi kwa wale iliyowauma poleeeni sanaaa, siku nyingine nitawashirikisha nikitaka kuposti, hivi kaka @loydemich mimi ni wakwanza kwani bongo kuvaaa hivi maeneo ya ufukweni?: mme wangu kaipenda balaaah yaani.


Irene Uwoya na Dogo Janja waliripotiwa kufunga ndoa Novembea 25, 2017, hata hivyo ni vigumu kutaja tarehe kamili kutokana na namna walivyoliweka suala hilo hasa kwa upande wa vyombo vya habari na mitandao kwa ujumla.

Comments are closed.