The House of Favourite Newspapers
gunners X

Uwoya: Bado Watu Hawana Majibu

0

SUPASTAA wa Bongo Movies, Irene Uwoya anasema kuwa, anajua watu wengi wanamchunguza kila kukicha kuhusiana na pesa zake na matanuzi anayoyafanya, lakini ukweli ni kwamba bado hawana majibu na kama wanayo ni ya uongo.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Uwoya anasema kuwa, anaamini kuwa watu wengi hata usingizi hawapati, kisa tu, wanataka kujua ni wapi anapata pesa na yuko na nani kwa sasa, jambo ambalo anasema watapoteza muda mwingi na hawatapata majibu.

 

“Najua wazi kuwa watu hawafumbi macho, wananitafakari tu bila sababu za msingi nab ado hawana majibu, lakini ukweli ni kwamba kupata majibu watachukua muda mrefu sana na watapoteza muda mno na hawatanijua, waendelee tu na kazi zao,” anasema Uwoya ambaye kwa sasa ndiye staa mwenye mkwanja mrefu na anayekula bata kuliko wote Bongo.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply