Itel mobile mapema leo imeungana na watoto wenye mahitaji maalum kwa kuonyesha upendo katika kuelekea msimu wa sikukuu za Eid Al Fitri.
Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es salaam na kuwakilishwa vema na balozi wa Itel Irene Uwoya ambapo wamejumuika na watoto yatima wa kituo cha CHAKUWAMA na kutoa zawadi mbalimbali.
Akizungumza mkurugenzi wa Itel Bw. Saimon Asajile amesema kuwa wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na kituo hicho cha kulelea watoto yatima na vinginevyo kwa kuhakikisha watoto wanakuwa na furaha na kupata mahitaji wanayostahili.
Kwa upande wake katibu mtendaji wa kituo hicho Bw.Hassan Khamis ametoa shukrani kwa Itel mobile na balozi wake kwa kuwakumbuka watoto hao kwa mahitaji muhimu.
Aidha amebainisha changamoto zinazowakabili watoto ni katika matibabu ya afya na kuiomba jamii iendelee kuweka ushirikiano ili kuwapa faraja watoto yatima.