UWOYA, J-LO NGOMA DROO KUDATE NA ‘WADOGO ZAO

Irene Uwoya

MSANII wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya anakuwa ngoma droo na mwanamuziki Jennifer Lopez ‘J-Lo’ kwenye suala zima la malavidavi na kudate na ‘wadogo zao’ baada ya kubainika kuwa wamewahi kudate na wanaume mbalimbali lakini wengi wao ni wadogo zao kiumri.  Tukianza na msanii wa Bongo Movie, Uwoya mwenye umri wa miaka 30 amewahi kuolewa na aliyekuwa mwanasoka marehemu Hamad Ndikumana. Baada ya ndoa yake hiyo kuvunjika akahamia kwa marehemu Ababuu. Alipotoka kwa huyo, waliobaki wote ni wanamuziki akiwemo Hamis Baba ‘H-Baba’, Msami Baby, Dogo Janja na Diamond.

Uwoya anaendana zaidi na J-Lo hapo kwenye suala la kuwazidi umri wanaume anaodate nao, mfano Uwoya alidate na Dogo Janja ambaye alimzidi miaka 10. Katika wapenzi wake wote huyu ndio alikuwa mdogo sana. Lakini pia alimzidi umri wa mwaka mmoja mwanamuziki Diamond huku pia ikielezwa kuwa, Msami ni mdogo sana kwa Uwoya licha ya kwamba haijafahamika ‘brazameni’ huyo ana umri gani.

Kwa upande wa J-Lo ambaye ni mwanamuziki, muigizaji na dansa naye amekuwa na uhusiano na ‘wadogo’ zake ambapo amewahi kudate na wanaume wengi lakini hapa nitakutajia ‘wadogo zake’ ambao ni Ben Affleck aliyekuwa amemzidi miaka miwili. Huyu alidate naye mwaka 2002 mpaka 2003.

J-Lo ambaye sasa ana umri wa miaka 49 pia ametoka na mwanamuziki mwenzake Aubrey Graham ‘Drake’, alimzidi umri kwa miaka 17, alidate naye miezi miwili tu kuanzia Novemba 2016 hadi 2017. Ojani Noa ni mwanaume ambaye J-Lo alidate naye akiwa amemzidi miaka mitano. Mwanamuziki mdogo zaidi aliyewahi kutoka J-Lo ni Casper Smart ambaye alimzidi kwa miaka 18. Penzi lao lilizua gumzo sana kama lilivyokuwa la Dogo Janja na Uwoya.

Ukiacha hao, J-Lo amewahi kubanjuka na wanaume mbalimbali, wapo aliofunga nao ndoa ambao walimzidi na wengine aliwazidi umri kama vile Marc Anthony, Cris Judd, Wesley Snipes, Chris Paciello na kwa sasa staa huyo anadate na Alex Rodriguez.

Toa comment