UWOYA KWELI KAFUNGA VIOO

Irene Pancras Uwoya

HATAKI shobo! Mwanamama sexy kunako kiwanda cha filamu za Kibongo ambaye ni mkali wa kupigilia pamba za bei mbaya kila kukicha, Irene Pancras Uwoya amesisitiza kuwa ni kweli muda umefika wa kuwafungia vioo watu ambao hawana manufaa kwake. 

 

Akizungumza na gazeti analolipenda la Ijumaa, Uwoya alisema anashangaa mno kuona mtu anamsema kuwa anaringa, lakini kumbe sivyo hivyo ameamua kudili na watu wenye faida kwake kwa sababu kuna watu wapowapo tu, hata asipowaona hakuna kinachopungua.

 

“Ni kweli kabisa nimeamua kuwafungia vioo watu ambao hawanisaidii chochote, yaani hawana mchango hata wa mawazo kwangu,” alisema Uwoya ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kiume, Krish.

Stori: Imelda Mtema, Dar


Loading...

Toa comment