Uwoya: Naye Ahofia Nyakunyaku!

lpKUMBE siyo Zari tu anayeogopa nyakunyaku! Hebu msikie staa wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya, naye anasema ni jambo la hatari mno kumuanika bwana’ke mpya kwani anahofia nyakunyaku watamnyakua.

 

Uwoya ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, mtu akimposti mwanaume wake anakuwa na wasiwasi kwamba atachukuliwa hivyo ili kukwepa presha zisizokuwa za lazima ni bora wasimjue badala yake wabaki kumsikia tu.

 

“Sithubutu kumwanika, nimejifunza kutokana na makosa hivyo wabaki tu kusikia ni yule au yule maana nyakunyaku wa mtandaoni hawana dogo,” amesema Uwoya ambaye mpaka sasa haijajulikana kama Oktoba 26, mwaka huu ni harusi yake au la.

STORI: IMELDA MTEMA,DAR


Loading...

Toa comment