The House of Favourite Newspapers

UWOYA NOMA AWAKALISHA WEMA, AUNT

HII ni noma! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya staa wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya kufanya kufuru ya aina yake na kuwakalisha mastaa wenzake, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel.

 

UWOYA ameonekana kuwakalisha Wema na Aunt baada ya kuteketeza mamilioni ya fedha katika matengenezo ya baa yake inayojulikana kwa jina la New Last Minute Lounge iliyopo Sinza jijini Dar ambayo matengenezo yake yamechukua muda mfupi.

 

Wema na Aunt wamekalishwa na Uwoya kwani biashara zao wanazozifanya haziwezi kufikia hatua aliyonayo Uwoya kwani Wema anamiliki duka la nguo za watoto huku Aunt akimiliki baa ambayo siyo ya hadhi hiyo. Baa hiyo ya Uwoya inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho ambapo watu mbalimbali pamoja na mastaa watakuwepo kushuhudia ilivyo ya hadhi ya kistaa.

Amani lilifanikiwa kufika kwenye baa hiyo yenye eneo kubwa na kujionea vitu vingi vya thamani na vya kisasa huku ulinzi wa eneo hilo ukiwa umeimarishwa kwani haruhusiwi mtu yeyote kukatiza ama kuingia eneo hilo kama hana kitu cha muhimu cha kufanya. Miongoni mwa vitu vya thamani vilivyomo ndani ni pamoja na viti, meza na masofa ya kisasa, jiko zuri la kupikia na kuchomea nyama, sehemu nzuri ya vinywaji na vingine vingi.

Ndani ya baa hiyo pamoja na kuwa na vitu vya thamani pia kuna vinavyoshangaza kwani ukutani kumepambwa na picha za mastaa mbalimbali ambao wameshafariki dunia akiwemo aliyekuwa rafiki yake kipenzi, marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’, Rachel Haule, Bi Kidude, Steven Kanumba, Albert Mangwea ‘Ngwea’, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’, Adam Kuambiana, Langa Kileo, Sharo Millionea na wengine wengi.

Mbali na picha hizo pia kuna sehemu tatu nzuri na zenye utulivu kwa ajili ya kunywea vinywaji na vyakula, ambapo mteja akikaa hawezi kuboreka kwani kuna hali ya hewa nzuri, TV kubwa yenye inchi 42. Baada ya Amani kutalii ndani ya baa hiyo, waandishi wetu waliweza kuzungumza mawili matatu na walinzi kuhusiana na uzinduzi utakavyokuwa;

Amani: Hongereni maana mandhari ni ya kishua sana.

Mlinzi: Unashangaa palivyo leo wakati hapa bado kuna baadhi ya vitu havijawekwa na wala viti vingine havijafunguliwa kama unavyoona vile pale kwenye maboksi yake, mambo bado hapa tukutane Ijumaa.

Amani: Kwa hiyo patakuwa moto eeh?

Mlinzi: Balaa, hiyo Ijumaa patakuwa hapatoshi kabisa yaani mji mzima unahamia hapa kwenye chimbo jipya lakini pa kishua kama ulivyosema (huku akicheka).

Amani: Ijumaa hiyo itakuwa ni kuanzia saa ngapi ili tufike?

Mlinzi: Nyie muwahi mapema ili msikose nafasi yaani mjitahidi kwenye saa saba mchana hivi muwe mshafika maana patakuwa hapatoshi hapa.

Amani: Hivi anaweza akawa ametumia kama shilingi ngapi kupapendezesha hivi?

Mlinzi: Hela nyingi (anacheka) siwezi kujua kiasi gani ila hata wewe si unaona vitu vilivyomo ni vya gharama, viti vya kisasa, chini mawe haya bei yake siyo ya kitoto yaani humu hauli vumbi, ukiingia huhisi joto maana kuna feni kama zote, ukijipanga lazima utapata vitu vizuri kama hivi.

Amani: Haya sisi tunaenda tutarudi tena Ijumaa kujionea mambo.

Mlinzi: Haya karibuni sana.

Alipovutiwa waya Uwoya kuzungumzia baa yake hiyo hakutaka kuanika gharama alizotumia zaidi ya kueleza tu anaizindua rasmi Ijumaa (kesho).

Stori: Memorise Richard na Shamuma Awadhi, Amani

Comments are closed.