The House of Favourite Newspapers

UWOYA: Tatuu ya Masogange Haijaniuma!

Irene Uwoya

STAA mkali wa filamu Bongo, Irene Uwoya amefunguka kuwa ‘tatuu’ aliyoichora kama kumbukumbu kwa rafiki yake kipenzi, video queen maarufu Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ haikumuuma hata kidogo tofauti na tatuu nyingine alizozichora mwilini mwake.

 

Akizungumza na Amani, Uwoya alisema kuwa kuchora tatuu hiyo mkononi mwake kunaonesha wazi Agness anaendelea kuishi ndani ya moyo wake siku zote na atamkumbuka sana kipindi chote cha urafiki wao wakati wa enzi za uhai wake.

“Nimechora tatuu ya Masogange sikuhisi maumivu kama niliyosikia nilipochora tatuu nyingine mwilini mwangu, nafikiri ni kutokana na uchungu mkali niliokuwa nao na kingine ni kwamba nimechora jina hili mkononi mwangu najua kila nikiliangalia nitapata amani ya moyo,” alisema Uwoya

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.