UWOYA USISAHAU KUTESA KWA ZAMU

Irene Pancras Uwoya

IRENE Pancras Uwoya ni mmoja wa wanawake warembo walioipa platfom’ tasnia ya fi lamu za Kibongo.   Mbali na kuigiza, Uwoya aliyezaliwa jijini Dodoma, Desemba 18, 1988 ni mwanamitindo, prodyuza na mwongozaji wa fi lamu za Kibongo. Alianza kujihusisha na sanaa mwaka 2007 baada ya kushiriki  kinyang’anyiro cha Miss Tanzania mwaka 2006 ambapo alishika nafasi ya tano.  Uwoya alifahamika sana kwa jina la Oprah baada ya kufanya vizuri kupitia Filamu ya Oprah ya mwaka 2008. Aling’ara mno kipindi hicho akiwa na waigizaji wakubwa kama marehemu Steven Kanumba na Vincent Kigosi ‘Ray’.

FILAMU

Mbali na Oprah, baadhi ya fi lamu alizocheza Uwoya na kufanya vizuri ni pamoja na Uliyemchokoza Kaja, Figo, Rosemary, Snitch, The Return of Omega, Money na nyingine zaidi ya 25 hadi sasa.

MAPENZI

Kwa upande wa uhusiano, Uwoya amepata kutoka na wanaume kadhaa. Aliingia kwenye ndoa na marehemu Hamad Ndikumana ‘Kataut’ aliyekuwa mwanasoka wa Rwanda. Alizaa naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Krish. Baada ya kutoka kwa Ndikumana, Uwoya alidai kufunga ndoa iliyoibua utata na msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’. Hadi unasoma hapa ndoa hiyo imedumu kwa mwaka mmoja tu na sasa kila mmoja ana maisha yake.

YAFUATAYO SASA…

Huyo ndiye Uwoya. Kuhusu uzuri wake, nani anatia shaka? Akikatiza mitaa ya Kinondoni au Sinza huwa vijana wanavunja shingo kumtazama. Ni kutokana na lile umbo lake matata lililokwenda hewani. Jipya ni lipi? Kwa sasa Uwoya mambo yake ni safi . Yaani mkwanja au mshiko umemtembelea kama wote. Achana na kipindi kigumu cha Januari au utawala wa Uncle Magufuli kama wengi wanavyosema vyuma vimekaza! Kwa Uwoya hajui hilo, badala yake anakula bata hadi kuku wanaona wivu!

GANDA LA NDIZI

 Watoto wa mjini wanasema Uwoya amekanyaga ganda la ndizi yaani anateleza tu. Akijisikia wikiendi hii kuwa Dubai kula bata ndivyo anavyofanya. Kuhusu magari na nguo za bei mbaya? Uwoya humwambii kitu. Anabadilisha magari kama nguo. Asubuhi unamuona na Toyota Mark X na jioni ana Mercedes Benz. Anatupia nguo za bei mbaya yakiwemo magauni ya hadi shilingi milioni moja kwa gauni moja.

Kuhusu pati? Uwoya anawachukua rafi ki zake kadhaa wanaenda kutafuna vyakula vya baharini visiwani Zanzibar au anakodisha boti na kuzunguka nayo kwenye Ufukwe wa Bahari ya Hindi wakila na kunywa hadi kunakucha. Ni rahisi tu kufanya birthday yake kwa gharama ya shilingi milioni 15 kwa usiku mmoja ambapo watu wake wanakula, kunywa hadi kusaza.

SWALI… 

Swali ni je, inakuwaje? Uwoya anapata wapi jeuri hii inayosababisha kina Maria Kijiko na Vero Mwenda kukosa usingizi wakiamini fi lamu zinalipa? Mabinti wa sasa mitaani hasa uswahilini hawataki kufanya kazi, wanataka kutoka kisanii. Wanataka kufanana na mtu mwenye ‘wadhifa’ kwenye jamii na kikubwa ni mume wa mtu. Mwenyewe Uwoya ukimbana maswali juu ya nani anampa jeuri hiyo anaishia kuchekacheka!

KUTESA KWA ZAMU

Ninachotaka kumwambia Uwoya ni kwamba anapaswa kujua kwamba kwenye ulimwengu wa mastaa huwa kuna kutesa kwa zamu hivyo sasa hivi ni zamu yake. Uwoya asisahau kwamba Jacqueline Wolper alipitia humo akiwa na yule Mkongo wake aliyempa jeuri ya kufa mtu. Wolper alikuwa anaangusha pati kila kukicha. Hakukumbuka hata kununua kiwanja wala kujenga hadi mkwanja ulipokata na sasa ametulia na ujasiriamali wa ushonaji nguo pale Kinondoni- Mkwajuni! Uwoya anapaswa kumkumbuka yule Wema Sepetu alipokuwa na kigogo CK. Wema alikuwa anamwaga fedha kama hana akili nzuri. Kila siku ilikuwa ni pati na kubadilisha magari na magauni ya bei mbaya. Wema alishatinga gauni lenye gharama ya shilingi milioni 3.

Baada ya jeuri kwisha sasa Wema ni mjasiriamali, anasimamia duka lake la nguo za watoto pale Mwananyamala-Komakoma. Hali ndivyo ilivyokuwa kwa kina Aunt Ezekiel, Tunda Sebastian na wengine. Uwoya anapaswa kujifunza wenzake walipokosea na asifanye makosa. Simshauri kwamba kudanga ni jambo jema, lakini ninamshauri kufanya uwekezaji mkubwa ili uwekezaji huo umsaidie

baadaye. Angalau afufue haraka ile biashara yake ya klabu ya starehe ya usiku pale Sinza- Mori, anunue kiwanja, ajenge nyumba yake ili aachane na nyumba za kupanga kwa staa mkubwa kama yeye. Pia anaweza kuangalia namna ya kujiendeleza kielimu kwenye fani yake ya fi lamu kwani ujuzi atabaki nao baada ya kigogo guyo kusepa kwani experience (uzoefu) unaonesha huwa hawadumu sana! Uwoya wewe ni mjanja, shtuka isile kwako kama wenzako!

Makala: Sifael Paul

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO


Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment