UWT Taifa Yawahasa Vijana Kuwa Wazalendo
Jumuiya ya umoja wa wanawake Taifa (UWT) imewahasa vijana na wanafunzi wa shule mbalimbali hapa nchini kuwa na uzalendo ili kutumikia nchi yao hususani wanaomaliza kidato cha sita na kupata nafasi ya kwenda katika mafunzo ya jeshi la kujenga Taifa .
Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Baraza kuu la UWT Taifa Lucy Edward Mwakyembe kwa niaba ya Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatada baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa katika shule ya sekondari Chabalisa iliyopo kata ya Nyabiyonza wilaya ya Karagwe vilivyoghramu milioni 100.
Akizungumza na wanafunzi pamoja na wananchi katika shule hiyo Mwakyembe amesema kuwa baadhi ya vijana wamekuwa na tabia ya kukataa kwenda jeshini kwa kusingizia kuwa ni mateso ambapo usababisha kukosa uzalendo na kujiingiza katika matendo yasikuwa na maadili ya Kitanzania ikiwemo Ushoga na Usagaji.
“Wazazi tushirikiane kuwaelimisha watoto kutojihusisha kabisa na utamaduni wa nje ambao si maadili ya Kitanzania kama vitendo vya Ushoga na Usagaji,watoto wetu wakiaribika awatapata wanawake au wanaume wa kuoa na kuolewa kwahiyo ni muhimu wazazi tubebe swala hili kwa umuhimu mkubwa” alisema Mwakyembe
Aidha amewahasa wanafunzi wa shule hiyo kujikita katika masomo na kutokubali kujiingiza katika matendo maovu na kutambua elimu ndo nguzo muhimu katika maisha huku akiwataka wazazi na walezi kupinga vikali ukatili wa kijinsia ambao umeshamili katika baadhi ya maneno hapa nchini.
Kwa upande wake Katibu Msaidizi Mkuu Utawala UWT Taifa Ndg Jenifer Chingulile amesema wapo baadhi ya wazazi ambao wanawakataza watoto kwenda kujiunga na jeshi la kujenga Taifa (JKT) pindi wanapomaliza kidato cha sita wakizani kuwa ni kwenda kupoteza muda jambo ambalo sio sahihi.
“Serikali inayoongozwa na chama cha mapinduzi Ccm haiwezi kupoteza fedha kuwapeleka vijana jeshini pasipo kuwa na faida hivyo ni muhimu vijana hususani waliomaliza kidato cha sita kwenda jeshini kujifunza uzalendo na kujifunza maadili mema ya Kitanzania na kujiepusha na suala la ushoga na usagaji” Alisema Jenifer.
Hata hivyo wananchi wa kijiji cha Nyabiyonza walipata nafasi ya kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo changamoto ya vitambulisho vya NIDA ambapo Mjumbe Baraza kuu la UWT Taifa ameahidi Chama cha mapinduzi CCM kitazitatua changamoto hizo.
Jumuiya ya umoja wa Wanawake Taifa (UWT) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mary Chatada inaendelea na ziara ya kikazi mkoani kagera ambayo ilianza mapema wiki hii kwa kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za Wananchi.