The House of Favourite Newspapers

Uzinduzi Wa Ligi Ya Upendo Super Cup Si Mchezo, Maendeleo Bank Wanogesha Mambo

0
Mwenyekiti wa Vijana Kanisa la KKKT Mabibo External na mratibu wa ligi hiyo, Erick Kisaule.

Dar es Salaam 21 Mei 2023: Uzinduzi wa Kombe la Upendo Super Cup linaloshirikisha sharika mbalimbali za Kanisa ya Kanisa Kiinjili Kilutheri jijini Dar es Salaam umefanyika katika Viwanja vya Mabibo Makuburi jijini na kushirikisha timu 14 ambazo zitatifuana.

Katika kunogesha michuano hiyo, Benki ya Maendeleo ambayo nayo inashiriki ligi hiyo imeahidi kudhamini michuano hiyo kwa ujumla na kuandaa zawadi nono kwa timu itakayoibuka na ushindi.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa ligi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangaraba alisema;

Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangaraba akizungumza na vyombo vya habari kwenye uzinduzi huo.

“Tunamshukuru Mungu leo kutukutanisha mahali hapa kushuhudia uzinduzi huu wa ligi hii ya Upendo Super Cup ambayo imeandaliwa na vijana wetu wa Mabibo External KKKT nasi kama Maendeleo Bank tumekuja kujiunga nao kwasababu nyingi tu.

“Moja ya sababu hizo ni jambo la faraja sana kuona vijana wanakusanyika mahali pamoja kwa jambo la baraka kama hili, wakifanya mazoezi, wanafahamiana, wanabadilishana mawazo na kujifunza mambo mbalimbali ya kimaisha.

Kamati ya maandalizi ya ligi hiyo kwenye picha ya pamoja mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani).

“Ni jambo la baraka umati kama huu kukusanyika mahali kama hapa kulikoni muda huu wangekuwa sehemu za ulevi, uharifu au sehemu zingine za hovyo.

“Kwa kusema hayo nipende kusema kuwa sisi Maendeleo Bank tumekuwa na ukaribu sana na vijana kwasababu vijana ndiyo nguvu ya kanisa, nguvu ya taifa na vijana ukiwaweka sawa katika maisha yao inasaidia sana nchi kusonga mbele kwa ustawi ulio bora hivyo tunawaomba vijana wengine popote walipo waige mfano huu.

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Goodluck Nkini akikagua timu kabla ya kipute kuanza.

“Nasi kama Maendeleo Bank timu yetu inashiriki na kudhamini michuano hii, lingine kubwa ni kwamba mwaka huu benki hii inatimiza miaka 10, hivyo tumeungana na vijana wa Mabibo External KKKT kuandaa mbio za Marathon ambapo ni muendelezo wa Upendo Super Cup kwasababu yote haya ni sehemu ya mazoezi.

Mgeni rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank wakifurahia jambo.

“Marathon ya Maendeleo Bank inatarajiwa kufanyika tarehe 2 mwezi wa tisa mwaka huu hapa jijini Dar es Salaam, tunawategemea sana vijana wenye nguvu kama hawa waje waungane na mpendwa waziri mkuu wetu, Majaliwa Kassim Majaliwa ambaye atakuwa mgeni rasmi kwenye marathon hiyo”. Alimaliza kusema Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangaraba.

Katika uzinduzi wa Upendo Super Cup mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Goodluck Nkini Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ambaye waliwapongeza vijana wa Mabibo External KKKT kwa wazo lao hilo zuri na kukusanyika pamoja kimishezo huku wakimsifu bwana. HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply