Uzinduzi wa Nureen Forever Suluhisho la Warembo kwa Bidhaa Bora

Mmiliki wa duka hilo Nureen Masele (kulia) akimsaidia kuchagua viatu mmoa wa warembo aliyefika kwenye uzinduzi huo.

 

 

 

NUREEN Forever suluhisho la warembo kwa bidhaa bora, hayo yalithibitika Jumamosi iliyopita umati wa warembo walipofurika kwenye uzinduzi wa duka la bidhaa za warembo kama vile nguo za aina mbalimbali ikiwemo za mtoko, harusi, kitchen party, mikoba, pochi, viatu, na mazagazaga mengine ya urembo.

Kila mmoja akichagua kimfaacho dukani hapo.

 

 

 

Duka hilo la Nureen Forever lililopo Mikocheni kwa Mwalimu Nyerere, Dar walifurika warembo kutoka pande mbalimbali waliokuwa wakijipatia mahitaji yao ya urembo.

Baadhi ya waliokutwa dukani hapo wakigonga chiaaaz kutakiana afya njema.

 

 

 

Akizungumza na mwanahabari wetu mmilikiwa duka hilo aliyejitambulisha kwa jina la Nureen Masele amesema duka hilo linauza bidhaa zenye ubora na kwa bei inayoendana na mhitaji.

Mambo yakiendelea dukani hapo.

 

 

 

Nureen amesema ameamua kuwekeza duka hilo eneo hilo kwa ajili ya kumaliza changamoto za warembo ambao wamekuwa wakihangaika kutafuta vitu vilivyo bora bila mafanikio.

 

 

 

Alimalizia kwa kuwakaribisha warembo wote kufika dukani hapo kwa ajili ya kujipatia bidhaa zenye ubora ambazo wamekuwa wakihangaika kuzitafuta na pengine kuziendea nje ya nchi.


Toa comment