Uzinduzi wa Ripoti ya Mipango Endelevu ya Kampuni ya Wentworth Gas Ltd
4 Agosti 2022, Dar es Salaam. Kampuni ya Wentworth Gas Ltd leo imezindua Ripoti yake ya Mipango Endelevu ya mwaka 2021. Ripoti hii inachagiza Ripoti Kuu ya Mwaka 2021 ya Wentworth Resources Plc., ikitoa maelezo zaidi kuhusu utendaji kuhusiana na masuala muhimu ya mazingira, kijamii, na utawala (Enviromental, Social and Governance – ESG) wa mwaka mzima.
Ripoti hiiinafuata muundo uliyowekwana Bodi ya Usimamizi ya Viwango vya Mipango Endelevu (Sustainability Accounting Standards Board- SASB) na kuthibitishwa na mshauri wa kujitegemea aitwaye GHD Services Incorporated.
Ripoti hii inaelezea mtazamo wa Wentworth wa uendelevu kupitia mkakati wa uendelevu unaowiana na Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Goals -SDGs) ya Kimataifa unaozingatia nguzo 5 za kimkakati, ambazo ni:
- Kusaidia mpito wa nishati unaowajibika;
- Kuwezesha mabadiliko ya nishati;
- Kujenga nguvu kazi mbalimbali na za kijumuishi;
- Kuendeleza ukuaji kupitia ushirikiano; na
- Utawala dhabiti wa mazingira, kijamii, na utawala.
Kwa kusambaza gesi asilia, yenye kiwango cha chini cha kaboni nchini kwa ajili ya uzalishaji wa umeme na matumizi ya viwandani, Wentworth inachangia mageuzi ya nishati ya Tanzania kwa kuwezesha umeme wa bei nafuu Tanzania; na pamoja na uwekezaji katika miradi ya elimu, afya na maendeleo ya kitamaduni, Kampuni inatoa mabadiliko chanya katika jamii.
Wentworth inaendelea kupunguza uzalishaji wake kaboni, baada ya kupata mojawapo ya viwango vya chini vya kaboni kwa mlingano wa kila pipa la mafuta (Barrel of Oil Equivalent –BOE) katika sekta mafuta na gesi ukilinganisha na makampuni yenye ukubwa kama wetu yaliyoorodheshwa kwenye soko dogo la hisa la London (AIM-listed). Aidha, Wentworth imetangaza ushirikiano wa makubaliano kupitia ubia wa muda mrefu na kampuni ya Vitol, ili kuendeleza miradi inayolenga jamii ambayo inatoa manufaa yanayolingana na Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa jamii ndani ya Tanzania.
Wentworth ni kampuni inayojitegemea iliyoorodheshwa na katika soko dogo la hisa la London (AIM-listed) na mshirika katika washirika wa Mnazi Bay pamoja na TPDC, Maurel &Prom. Maelezo zaidi ya ripoti hii yanapatikana katika ripoti yetu ya Mipango Endelevu ya mwaka 2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wentworth Resources PLC, kampuni mama ya Wentwoth Gas Limited, Katherine Roe alisema kupitia historia yetu mahiri, mtindo thabiti wa biashara na ufanisi mkubwa wa kifedha Wentworth inazalisha gesi ili kuivusha Tanzania katika uchumi wa kesho.
“Ninafuraha kuthibitisha kwamba Wentworth Resources PLC inaunga mkono Kanuni Kumi za UmojaMkataba wa Kimataifa (United Nations Global Compact) kuhusu haki za binadamu, kazi, mazingira, na kupambana na rushwa. Tumejitolea kuzifuata kanuni hizi za Umoja wa Mataifa na kuwa sehemu ya mkakati, utamaduni na shughuli za kila siku za kampuni yetu, na kushiriki katika miradi shirikishi inayoendeleza malengo mapana ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa, hasa Malengo ya Maendeleo Endelevu. Pia tunashirikiana na serikali ya Tanzania kuunga mkono agenda yake ya maendeleo ya taifa katika nishati na mazingira. Na kwa kufanya hivyo, tunaboresha maisha ya watu” – Mkurugenzi Mtendaji, Wentworth Resources PLC, Katherine Roe.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Frank Morandi, Simu: +255783 211 123 au Barua pepe: [email protected]