The House of Favourite Newspapers

UZUNGU WADAIWA KUMFELISHA BELLE 9

Abedinego Damian, ‘Belle 9’

MWANAMUZIKI ambaye amefanya mambo mengi kwenye gemu la Bongo Fleva ikiwa ni pamoja na kutengeneza kolabo kali, Abedinego Damian, ‘Belle 9’, amefungukia madai ya kwamba Uzungu kwenye ngoma zake unamfelisha kimuziki hayana ukweli wowote na wanaozungumza wanafuata tu mkumbo.

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Belle 9, ambaye anatamba na Ngoma ya Take Away, alisema kwanza hajafeli kimuziki, nyimbo anazotoa zinakubalika sana na muziki ni hisia hata uimbe lugha gani kama unakipaji watu wanaelewa kile unachoimba.

“Lugha kwenye muziki inanafasi ndogo sana kuliko kipaji cha mtu na uwezo wake. Kuna nyimbo za Kikongo hapa zinasikilizwa sana na watu utasema wanaelewa Kikongo au Kilatino. Muziki unazungumza na mtu yeyote kwa lugha yoyote ile kwa hiyo madai hayo hayana mashiko, mashabiki zangu waendelee kunisapoti na kufurahia muziki mzuri kutoka kwangu,” alisema Belle 9.

BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.