Vai adai hana sifa za mke

Imelda Mtema

KATIKA hali ya kushangaza, msanii wa filamu asiyeishiwa vituko, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ amekiri kuwa tabia zake za kulewa kila siku zinamfanya kukosa sifa za kuwa mke wa mtu.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Vai alisema ameshazoea kupiga ulabu hata akiamka asubuhi, kitu kinachomshawishi kuamini kuwa ni vigumu kumpata mwanaume atakayekubali kuishi na mwanamke wa aina hiyo.

“Suala la mimi kuolewa au kuwekwa ndani ni ngumu, maana tabia zangu hazisomeki, mume mwenyewe atanitema haraka sana. Naona bora nikae hivihivi isije ikawagharimu wazazi wangu kurudisha mahari ya watu,” alisema Vai.


Loading...

Toa comment