The House of Favourite Newspapers

‘SIKU YA WAPENDANAO’ ILIVYODAMSHI NDANI YA DAR LIVE

Khanifa Maulid au “Jike la Chui”,  mmoja wa waimbaji wa muziki uliotoa burudani  Siku ya Wapendanao jana (Februari 14) katika  Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ulioko kitongoji cha Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam..

USIKU wa kuamkia jana ulimwengu ulisherehekea Siku ya Wapendanao ambapo katika Jiji la Dar es Salaam moja ya sherehe kubwa za kuadhimisha siku hiyo nchini, ilifanyika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ulioko kitongoji cha Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

Uwanja huo ulijaa kila aina ya nuru za watu, nguo na vitu, zikiwemo zawadi mbalimbali kuadhimisha siku hiyo inayochochea upendo kwa watu wanaopendana.

Wakati wote huo wapendanao hao walikuwa wakichombezwa na nyimbo za kimahaba kutoka kwa mkali wa nyimbo za kubembeleza, Beka Ibrozama, aliyekuwa akibadilishana jukwaa na mkali wa nyimbo za kimahaba zenye mahadhi ya kimwambao.

Wengine walionogesha mambo ni kundi la YAH TMK Modern Taarab na Khanifa Maulid ‘Jike la Chui’.

Patricia Hillary akiimba kibao cha ‘Njiwa Peleka Salamu’.
Shabiki akijimwaya na Patricia jukwaani.
Mtangazaji wa kipindi cha Ng’aring’ari cha Kituo cha televisheni ya Clouds, Sakina Lyoka (wa tatu kushoto akiwa na mkono kifuani), akishiriki  kuiremba siku hiyo.
…Akimlisha keki Patricia.

PICHA: RICHARD BUKOS / GPL     

Comments are closed.