The House of Favourite Newspapers

VANESSA AJIBU ISHU YA KUMWAGANA NA JUX

Vanessa Mdee ‘Vee Money’

MWANADADA anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ kwa mara ya kwanza ameibuka na kufunguka kuhusu madai ya kumwagana na mpenzi wake, Juma Jux.

Akibonga na Za Motomoto News mrembo huyo baada ya tetesi kuzagaa amemwagana na Jux kwa sababu amemsaliti alisema hana tatizo kabisa na Jux ila kazi ndiyo zinazowafanya wasiwe karibu hivyo watu kuona kama hawapo sawa.

“Mimi na Jux hatuwezi kuwa pamoja kila siku kuna kipindi kazi zinabana sana na ndio maana watu wanaona tumemwagana, niwatoe hofu tu mashabiki zangu kwamba tupo sawa na hakuna kitu chochote kibaya kinachoendelea kati yetu zaidi ya ubize wa kazi unaotufanya tuwe mbali,” alisema Vaness

Stori: Memorise Richard, Dar

Comments are closed.