The House of Favourite Newspapers

Vanessa Mdee Aachiwa Kwa Dhamana

Habari zilizotufikia hii punde, zinaeleza kwamba msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Bongo, mwanadada Vanessa Mdee ‘V-Money’ aliyekuwa akishikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi (Sentro) kwa tuhuma za kuhusika na matumizi/biashara ya madawa ya kulevya, ameachiwa kwa dhamana.

Taarifa zilizothibitishwa na meneja wake aliyefahamika kwa jina moja la Seli, ameuambia mtandao huu kwamba V- Money ameachiwa kwa dhamana.

V-Money anaingia kwenye orodha ya mastaa Bongo, waliosota mahabusu, baada ya kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, katika orodha ya watu waliotakiwa kujisalimisha Sentro, kwa tuhuma za kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.

Habari zaidi zitaendelea kukujia kupitia hapahapa.

Comments are closed.