The House of Favourite Newspapers

#GlobalUpdates: Vanessa Mdee Kuachia Wimbo Mpya Wiki Hii Na Kutumbwiza Kwenye ‘Gidi Fest’ Nigeria

Kwa misukosuko aliyoipitia Vanessa Mdee hivi karibuni sio rahisi kufikiria kuwa msanii huyo ana nguvu ya kuachia kazi mpya kwa sasa, lakini kwa mujibu wa tweets zake za jana ni wazi kuwa changamoto alizokumbana nazo zimempa morali kubwa zaidi…

Akiwa miongoni mwa wasanii waliotajwa kwenye list ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, Vanessa Mdee siku ya Machi 13 2017 aliachiliwa kwa dhamana na siku mbili badaae alirdui mtandaoni kusema na mashabiki wake. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Vee Money aliwashukuru mashabiki kwa kuonyesha upendo mkubwa juu yake na kusema tutegemee kazi mpya kutoka kwake wiki hii:

Kama ulikuwa unawaza juu ya maendeleo yangu. Naendelea vizuri sana. Isitoshe ngoma mpya inatoka WIKI HII ” – Alisema Vanessa kupitia Twitter page yake. 

Kuzisoma tweets zote za Vanessa Mdee, bonyeza hii link ya blue ikupeleke moja kwa moja kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Licha ya kutegemea kazi mpya kutoka kwa ‘Cash Madame’, Vanessa Mdee ataungana na msataa wa Nigeria kama Davido, Burna Boy, Seyi Shay na Reekado Banks wa Mavin Reords kutumbwiza kwenye tamasha kubwa la muziki nchini humo ‘Gidi Fest’ linalotegemea kufanyika mwezi wa nne kwenye msimu wa sikukuu za pasaka.

Kwa sasa unaweza kumpata Vanessa Mdee kwenye msimu wa tano wa series ya MTV Shuga Down South inayoruka kupitia chanel ya MTV Base na BET kwenye kingamuzi cha DSTV.

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.