VEE MONEY, JUX WAITIKISA BURUNDI

Juma Musa ‘Jux’

MASTAA wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee na Juma Musa ‘Jux’ wameitikisa Burundi ambapo mapokezi yao tu yalikuwa ya kifalme.

 

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo wakazi wa Bujumbura walijitokeza Uwanja wa Ndege Bujumbura wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali zinazoonesha ni jinsi gani wanawakubali wasanii hao.

 

Licha ya mabango hayo, Vanessa na Jux walipokelewa na msafara mkubwa wa magari pamoja na mashabiki kibao ambapo baada ya hapo waliwakonga nyoyo kwa shoo kali iliyofanyika katika Fukwe za Lacosta.

 

Vanessa na Jux wako kwenye mwendelezo wa ziara yao ya In Love and Money wanayoifanya ndani na nje ya Tanzania. Akiwa nchini humo Vanessa alisema ni mara ya kwanza kufika Burundi na ameshangazwa na mapokezi makubwa ambayo hakuwahi kuyafikiria.

Toa comment