The House of Favourite Newspapers

Vee Money, Khadija Kopa kuwadindikiza jahazi Dar Live

0

mdeeaVanessa Mdee ‘Vee Money’

STAA wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ pamoja na Malkia wa Taarab, Khadija Kopa wanatarajiwa kuwasindikiza wakali wa muziki wa Taarab, Jahazi Modern katika uzinduzi wa albamu yao ya Kaning’ang’ania, Januari 30, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.

6 Malkia wa Taarab, Khadija Kopa.

Akichonga na Amani mratibu wa shoo hiyo, Seif Magwallu ‘Shiboli’ alisema kuwa usiku huo Khadija Kopa ataambatana na kundi lake la Ogopa Kopa huku Vee Money akiwa na madansa wake ambao ni habari ya mjini.

“Mashabiki watambue, Jahazi huwa hawakosei siku zote, baada ya kufanya uzinduzi wa kihistoria katika Albamu ya Chozi la Mama safari hii mashabiki watarajie utofauti kutoka kwa wakali ndani ya albamu mpya ambao ni Mzee Yusuf, Mwanakhamis Mohamed ‘Miss Jahazi’ Fatuma Kassim, Leila Rashid pamoja na Fatuma Ally,” alisema Shiboli na kumalizia kuwa kiingilio kitakuwa shilingi 10,000 tu getini.

Leave A Reply