The House of Favourite Newspapers

Vera, Daktari Bongo… Mahaba Kama Yote – Pichaz

0

 

 AMKENI, amkeni jamaniii! Habari ya mjini ni penzi zito la mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Vera Sidika na daktari Mbongo Jimmy Chansa.

 

Habari ilianza kama upepo wa kisulisuli kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwahusisha wawili hao katika mapenzi huku wakionekana katika picha wakijirusha sehemu mbalimbali duniani ikiwepo Dubai, Falme za Kiarabu.

Kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya, hakusita kuweka wazi penzi lake na Chansa lakini kwa daktari huyo kumekuwa na hali ya utofauti.

 

HUYU HAPA CHANSA

Risasi Mchanganyiko lilipomtafuta Chansa kwa njia ya simu ili azungumzie uhusiano wake na Vera alisema:

“Mambo yangu na Vera huwa sipendi kuyaongelea kabisa.”

Alipoulizwa kwa nini hapendi kuyaongelea mapenzi hayo wakati kila kitu kiko kwenye mitandao na hasa nchini Kenya, alisema: “Ndiyo najua lakini mimi si mtu wa kuweka wazi mambo yangu binafsi.”

 

PENZI LAWA GUMZO

Kutokana na picha zao za kimahaba kuenea mitandaoni, gumzo la penzi hilo lilikuwa kubwa hasa kufuatia wanaume mastaa Bongo kunasa kwenye penzi la wanawake wa Kenya.

“Naona mashemeji wanazidi kuongezeka, hongera wadada wa Kenya kwa kuwavutia wakaka wa Magufuli (Rais John Magufuli) najua mnatengeneza umoja mpya,” mmoja kati ya wachangiaji kwenye mitandao ya kijamii Kenya aliandika posti yake kwenye mtandao wa Instagram uliokuwa na ishu ya penzi la Chansa na Vera.

 

Wakati gumzo hilo likiendelea nchini Kenya, Bongo nako mambo hayakupoa kwani wengi walitafsiri penzi hilo kama safari ya daktari huyo (jina la hospitali anayofanyia kazi limehifadhiwa) kutafuta sapoti kwa mwanamke huyo kama alivyofanya msanii Bernard Paul ‘Ben Pol’ ambaye amejiweka penzini kwa mwanamke tajiri wa Kikenya aitwaye Anerlisa Muigai, msichana tajiri anayemiliki Dola za Kimarekani bilioni moja (zaidi ya shilingi trilioni 2.3).

 

UTAJIRI WA VERA SIDIKA

Vera ni mwanamitindo, mjasiriamali ambaye amezaliwa Septemba 30, 1989 anayekadiriwa kuwa na utajiri wa dola za Kimarekani milioni 2.5.

 

Mwanamitindo huyo anadaiwa kumiliki gari aina ya BMW X5 yake yenye thamani ya shilingi milioni 6.5 za Kenya, shamba kubwa la kuku, kipande cha Ardhi huko Kilifi, jumba la kifahari huko Kileleshwa ambako ndiko anakoishi.

Mwanamke huyo pia ametajwa kumiliki maduka ya kuuza vipodozi na duka la kuuza bidhaa mtandaoni linaloitwa Veescollection.

AHUSISHWA NA BIASHARA ZA SIRI

Mara kadhaa mwanamitindo huyo ameelezwa kuwa ni mwanamke anayeishi maisha ya kifahari huku akihusishwa kuwa na biashara zisizokuwa rasmi kwenye nchi mbalimbali kama Nigeria na Afrika Kusini.

 

VERA ASHINDWA KUJIZUIA

Awali kabla mambo ya penzi lake na Mbogo hayajawa moto, Vera alisemekana kuwa na mchumba raia wa Senegal lakini alipotua Bongo Agosti, mwaka huu alishindwa kujizuia pale alipofunguka mbele ya Televisheni moja nchini kuwa;

“Nimemfuata mpenzi wangu,” alisema Vera akimaanisha kumtaja Jimmy.

 

JIMMY NI NANI?

Mbali na kuwa ni daktari maarufu kwenye hospitali kongwe hapa nchini, Jimmy ametajwa kuwa ni msanii ambaye katika siku za hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya ujulikanao kwa jina la Nakuwaza.

Hata hivyo ‘CV’ nyingine za daktari huyo zimekuwa gizani kutokana na wengi kutomtambua vyema ingawa Jimmy anaonekana kuwa ni mtu wa maisha ya ‘bata’ la kufa mtu.

 

JIMMY AONYWA

Pamoja na kupongezwa na baadhi ya watu kuwa katika uhusiano na mwanamke huyo tajiri nchini Kenya, baadhi ya watu wamemuonya Jimmy kuwa anapoendelea na safari ya penzi lake akumbuke na kutazama nyuma kwa madai kuwa huwenda Vera akammwaga siku zijazo.

 

“Yeye si mwanaume wa kwanza kuwa na Vera, ameshakuwa na uhusiano na wanaume wengi kutoka Kenya, Nigeria na kwingineko, lakini wako wapi? Aliwamwaga na leo anaendelea na maisha,” alisema mchangiaji mmoja kwenye mtandao wa kijamii.

 

Kama uhusiano wa Jimmy na Vera utadumu, basi daktari huyo Mbongo atakuwa amefuata nyayo za msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’, Ali Saleh Kiba ‘Ali Kiba’, Ben Pol ambao wamekuwa kwenye uhusiano wenye nguvu na wanawake Wakenya.

 

STORI |  IMELDA MTEMA, RISASI

Leave A Reply