The House of Favourite Newspapers

Vera Kufanya Tena Sajari ya Matiti

0

MREMBO maarufu mitandaoni nchini Kenya na Afrika Mashariki, Vera Sidika anasema atafanya tena sajari ya matiti yake ili kuboresha muonekana wake baada ya kuzaa.

Vera anasema anatamani kupata matiti yenye umbo la mviringo na ambayo yamesisima, mara tu baada ya kunyonyesha.

“Kunyonyesha hakujawahi kunisumbua hata kidogo, nafanya hivyo kwa kujivunia na nina furaha. Mara tu baada ya kumaliza kupata watoto, hakika nitafanyiwa upasuaji wa kubadilisha umbo la matiti yawe ya kuvutia, ya mviringo na yaliyoinuka,” anasema Vera.

Ikumbukwe Vera ambaye miaka michache iliyopita alifanyiwa upasuaji wa kuongeza ukubwa wa matiti yake pia ameweka wazi kwamba amekuwa akijivunia kumnyonyesha binti yake, Asia Brown aliyezaa na msanii Otile Brown.

Leave A Reply