#GlobalCelebrityUpdates: Vera Sidika Achoshwa Na Maisha Ya Kuishi Peke Yake, Adai Bora Kufanya Haya…
Baada ya kuweka wazi mahusiano yake na tajiri mmoja wa Nigeria aishie Dubai, socialite maarufu East Africa Vera Sidika anaendelea kuwa gumzo kwenye social networks.
Kwenye pita pita yangu mtandanoni nimekutana na Snapchat post ya Vera Sidika iliyonifanya niwaze kuwa pengine socialite huyo ameamua kweli kutulia na kuanzisha familia.Kwenye post hiyo, mwanadada huyo aliweka kikatuni cha mdada mwenye ujauzito na kudai maisha ya kuishi peke yake, kivyake vyake sio issue tena kwanza inaboa na pengine umeshafika wakati wa yeye kufanya mipango ya kuwa na watoto.
” Kuishi mwenyewe inaboa kinoma, its lonely. Ingekuwa bora kuwa na watoto wanaokimbizana huku na kule ndani ya nyumba na sio maisha haya…” – aliandika Vera Sidika.
Miezi michache iliyopita Vera Sidika alikuwa akipost picha nyingi kwenye Instagram zikumuonyesha akiwa Dubai anakula good life, miezi michache baada ya trip hiyo mwanadada huyo aliamua kuweka wazi kilichompeleka huko.
Kupitia Instagram page yake, Vera Sidika alipost picha ya boyfriend wake, aliyedai ni tajiri mmoja wa Nigeria aishie Dubai na kusema ndiye aliyekuwa nae kwenye vacation yake nchini humo.
Wewe unaonaje? Vera Sidika yupo serious… au ndio mipango?
IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.
Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, muziki na nyingine zikufikie kwa wakati.
Comments are closed.