VETA Waja Na Ubunifu Wa Saluni Ya Vipodozi Vya Matunda Halisi
Dar es Salaam 5 Julai 2024: Chuo Cha Ufundi VETA Shinyanga kimekuja na ubunifu wa vipodozi vya matunda ya asili ambavyo havina madhara katika miili ya binadamu kutokana na kutokuwa sumu za kemikali.
Akizungumza katika Maonesho ya Kibiashara ya 48 ya Kimataifa ambayo yanafanyika katoka Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini, Mwalimu wa Saluni, Mapambo, Urembo na Vipodozi, Judy Mwita amesema kuwa wamekuja na ubunifu huo kwa sababu ni wa asili na hauna madhara yoyote kwa mtumiaji.
“Huu ubunifu tumeona tuje nao ili kuwapa elimu wananchi wote ambao wanatutelea katika banda letu ili waweze kujifunza namna ya kutumia vitu vya asili mfano matunda, vitunguu, abdlasini, nazi papai, parachichi na vitu ambavyo ni rahisi kupatikana na visivyo na madhala yoyote,” amesema.
Hivyo basi amewakieibisha Wananchi wote kwa ujumla kutembelea katika banda la VETA ili kujifunza na kupata elimu kuhusu namna ya matumizi ya Urembo utokanao na vitu vya asili.