The House of Favourite Newspapers

Video: Kocha Yanga na Niyonzima Watamba “Hatuna Hofu na Simba”

0

NASSREDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga leo Mei 7, 2021 amesema kuwa anatambua kwamba timu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ni timu nzuri ila hana hofu kuelekea mchezo wa kesho Uwanja wa Mkapa.

Nabi kesho atakutana na Gomes wa Simba katika mchezo wa Kariakoo Dabi utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.

 

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 1-1 hivyo kesho utakuwa ni mchezo wa kukata na shoka kwa timu zote mbili kuwania pointi tatu.

Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya pili imekusanya pointi 57 na Simba ipo nafasi ya kwanza imekusanya pointi 61.

 

Nabi amesema:”Ninaitambua Simba, nimewahi kukutana nao kwenye Ligi ya Mabingwa hata kocha wao Gomes, (Didier) ninamtambua.

 

“Licha ya kwamba Simba ni timu kubwa sina hofu nao nina amini kwamba kila timu ina mbinu zake na aina ya kufanya katika kutafuta matokeo,” amesema.

 

Nahodha msaidizi wa Yanga Haruna Niyonzima amesema wamejiandaa vizuri kuelekea mchezo wa watani wa jadi ana anafahamu vyema kuwa mchezo mkubwa huchezwa na wachezaji wakubwa.

 

Kocha msaidizi wa Simba, Selemani Matola amesema licha ya kuwa ni mechi ya Derby lakini watacheza vizuri dhidi ya Yanga bila kubutua.

 

 

Leave A Reply