VIDEO: Msukuma Aomba Askari wa Kike Kwa Rais Magufuli

MBUNGE wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Msukuma,  leo ameomba polisi wa kike kwa Rais John Magufuli kwa ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali katika jimbo lake.

Msukuma amesema hivyo wakati wa uzinduzi wa nyumba za makazi ya Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita ambazo zitakuwa na uwezo wa kutumiwa na askari 30.

Alichokisema Msukuma: “Polisi ni marafiki zangu sana siwashtaki.  Nimezungumza bungeni.  Jimbo langu lilikuwa linaongoza kwa wakata mapanga, tukajitoa tukajenga kituo, sasa hakuna wakata mapanga.  Shida yangu ni moja tu, jimbo zima hakuna askari wa kike, lakini nikiomba askari wa kike naambiwa mgao, mara mazingira magumu.  Hivi nilivyo kweli nina mazingira magumu, watu wanakaguliwa na askari wa kiume na mnajua maumbile ya Wasukuma; ikikupendeza nipatie askari wa kike.”

Rais Magufuli anaendelea na ziara yake iliyoanzia mkoani Geita wiki iliyopita na sasa anaendelea mkoani Mwanza.


Loading...

Toa comment