The House of Favourite Newspapers

Video: Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa TANU Afunguka Mazito!

0


Mzee Dk. Fortunatus Lwanyantika Masha ambaye aliwahi kuwa Katibu Mwenezi wa TANU akafukuzwa Agosti 1968 amesema, hakujua kwa nini alitimuliwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumza na Global Tv, Sengerema, Mwanza, mzee Masha alisema mkutano wa Halmshauri Kuu ya TANU ulioketi Tanga ndio uliofanya uamuzi wa kuwafukuza chama bila kupewa nafasi ya kujitetea yeye na wenzake tisa.

“Kabla ya kufanyika mkutano ule mimi nilijua kuwa tutafukuzwa lakini nilidhani tutaitwa ili kujitetea lakini haikuwa hivyo,” alisema Dk. Masha.

Alisema baada ya kufukuzwa chama yeye na wenzake tisa akiwemo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Oscar Kambona aliamua kuishi kijijini kwao Sengerema kwa mwaka mmoja kabla ya kuamua kutafuta kazi.

“Nilitafuta kazi sehemu mbalimbali lakini nikawa naambiwa kwamba serikali imesema nisiajiriwe, hivyo nikaamua kwenda Marekani,” alisema.

Alifafanua kuwa alipofika huko alijiendelea kielimu mpaka akapata shahada ya udaktari na akaajiriwa Umoja wa Mataifa ambako alifanya kazi hadi alipostaafu miaka kadhaa iliyopita.

Kuhusu mwanaye, aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha kujiingiza kwenye siasa alisema alijua kuwa anaingia katika hatari kutoka na yeye kupata misukosuko mingi ya kisiasa lakini kwa kuwa mwanaye ni mtu mzima hakupinga maamuzi yake.

“Kwanza nilifurahi kuona ana moyo wa uzalendo kwa kurudi nchini na kutumikia taifa lake, lakini naamini niliwalewa vema na sasa wanathamini nchi yao. Kuingia siasa ni maamuzi yake, kwanza aliwahi kuwa waziri, mimi sikuwahi kufika ngazi hiyo, kwa hiyo anajua siasa ni nini,” alisema Dk. Masha.

HABARI: ELVAN STAMBULI | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply