Video: Bajeti Kuu Ya Serikali Yawasilishwa Bungeni Leo


LEO Juni 10, 2021 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Mwigulu Nchemba, amewasilisha Bungeni Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Waziri Mwigulu Nchemba amesema Makadirio ya matumizi kwa mwaka 2021 yalikuwa Trilioni 34.88 ambapo Trilioni 22.10 ni matumizi ya kawaida na Trilioni 12.78 ni Matumizi ya Maendeleo Katika kipindi cha Julai 2020-Aprili 2021 jumla ya Tsh. Trilioni 24.74 zimetolewa

 

“Mheshimiwa Spika, mlipuko wa Uviko 19, umesababisha kutofikiwa kwa baadhi ya malengo ya ndani hususan sekta za utalii, usafiri wa anga na uingizaji wa bidhaa kutoka nje,”

 

“Napendekeza kuanzia mwaka 2021/22, Serikali Kuu ianze kulipa posho za kila mwezi za waheshimiwa madiwani moja kwa moja tena kwenye akaunti zao kwa halmashauri zote zenye uwezo mdogo kimapato.”

 

“Napendekeza kulipa madeni yanayodaiwa na mifuko kwa kutenga fedha kwenye bajeti na kutumia utaratibu wa kutoa hatifungani maalum isiyo taslimu (Non- cash Special Bond) zitakazoiva kwa nyakati tofauti kuanzia miaka miwili hadi 25.”

 

“Kupunguza ushuru wa forodha hadi asilimia 0 kutoka asilimia 10 na asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi zinazotumika katika uzalishaji wa vifaa maalum vinavyotumika katika kupambana na UVIKO-19”

 

Kuanzisha tozo ya ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 10 kwenye pikipiki zilizotumika kwa zaidi ya miaka mitatu zinazoingizwa nchini ili kudhibiti uingizaji wa pikipiki chakavu na kulinda mazingira

 

“Mheshimiwa Spika kwa upande wa viashiria vinavyopima uwezo wa nchi kulipa deni, matokeo yalibainisha kuwa, uwiano wa ulipaji wa deni la nje kwa mapato ya ndani ni asilimia 13.7 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 23,”

 

“Napendekeza kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye simu janja za mkononi, vishikwambi (Tablets) na modemu (modems) ili kuhamasisha matumizi ya huduma za mawasiliano kufikia asilimia 80 ifikapo mwaka 2025 kutoka asilimia 46”

 

Mheshimiwa Spika, kuhusu uhimilivu wa deni la Serikali, tathimini iliyofanyika Novemba 2020 kwa mujibu wa sheria ya mikopo, dhamana na misaada sura namba 134, tathimini hiyo ilionesha kuwa, viashiria vya deni la Serikali viko ndani wigo unaokubalika kimataifa,”

 

Kusamehe kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye nyasi bandia kwa ajili ya viwanja vya Mpira vilivyoko kwenye majiji. Msamaha huo utahusisha ridhaa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania. Lengo la hatua hii ni kuendeleza michezo na kukuza vipaji nchini amesema Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCxTecno


Toa comment